Na John Mapepele
Waziri Wa Utamaduni, Sanaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amehimiza umuhimu wa kumuenzi mwanaharakati mwanamke, Bibi Titi Mohamed aliyefanya kazi kwa karibuni na Mwalimu Julisu Nyerere katika harakati za kuleta uhuru wa Tanganyika.
Akizungumzia tamasha la Bibi Titi Mohamed litakalofanyika wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, Mhe. Mchengerwa kwenye kipindi cha 360 cha kituo cha televisheni cha Clouds leo ambapo amesema Bibi Titi ni alama ya mabadiliko katika suala zima la ushiriki wa wanakwake katika harakati hizo na kuleta mabadiliko.
“Ukimzungumzia Bibi Titi Mohamed unazungumzia alama ya mabadiliko, unazungumia alama ya kutoka kutoamini kuja katika kuamini kwa sababu Bibi Titi mwenyewe aliamini kwamba tunaweza kujikomboa,” amesema.
Amesema ni vigumu kuzungumzia mabadiliko ya kisiasa ya kuwaingiza wanawake katika siasa, ushawishi wa katika siasa, uchumi, matumizi ya Kiswahili, bila kumzungumzia Bibi Titi Mohamed.
Amesema vijana wanaweza wasijue umuhimu wa Bibi Titi katika historia ya Tanzania kutokana na mifumo. "Inawezekana wapo vijana wa leo hawafahamu hata Mwalimu Nyerere alifanya nini."
Amesema taifa lolote linalotaka kupiga hatua, ni lazima waasisi na mambo makubwa waliyofanya yaandikwe.
Amemuelezea Bibi Titi kuwa alikuwa tayari kutoa maisha yake, kuacha ndoa yake kuhakikisha Watanzania wanakuwa huru. Vile vile aliacha madaraka yake kwa ajili ya kile alichoamini.
Kwa mujibu wa Mhe. Mchengerwa, Bibi Titi aliamini katika kufanya kazi kwa bidii na kuamini kwamba kila jambo linawezekana.
Ukimzungumzia Bibi Titi unazungumzia siasa ya Afrika Mashariki kwa sababu alifika kote huko. "
Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema nguvu ya ushawishi wa mwanamke ni muhimu katika kuleta mabadiliko ya maendeleo mbalimbali yakiwamo ya kiuchumi na kisiasa.
Ametoa mfano wa wanawake ambao wamekuwa na ushawishi na mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo akisema, upo msingi uliowezesha.
Ameongeza, “ kuwa na nguvu ya ushawishi wa mwanamke ni muhimu sana katika kuleta mabadiliko ya maendeleo…Ili tuweze kuwa huru, lazima tuwatumie wanawake.”“ Unapoungumzia Anna Abdallah aliyekuwa mwanamke wa kwanza kuwa Mkuu wa Mkoa nchini, unapozungumzia Anna Makinda aliyekuwa Spika wa kwanza mwanamke, Rais,Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwa rais wa kwanza mwanamke upo msingi ambao umeyafanya yote haya.
”Alisisitizia Na hapo tulipokosea ni kwa sababu historia yetu imewekwa kando inaweza ikawa sababu ya vijana wa leo uzalendo na utaifi kupungua. Hawajui amani hii iliyopo mambo gani yamefanyika na kuwa na maendeleo tuliyo nay o na wazee walijitoaje.