Waziri Simbachawene, Aongeza Ari Ya Ufaulu Sm Iramba

 Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amempongeza Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Iramba kwa kuongeza kiwango cha ufaulu wanafunzi wa darasa la saba.

Kauli hiyo ameitoa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika kata ya Rudi jimbo la kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa ambapo alifanya mkutano wa hadhara na kutembelea mradi wa maji.

“Ameweza kufaulisha wanafunzi 32 kati ya wanafunzi 40 baada ya kuwaahidi kwenda Bungeni Mjini Dodoma, wanafunzi hao wamefaulu kwa wastani wa daraja B na Daraja C.”

Watoto wanaakili sana ila wazazi wao wanawaambia wasifaulu kwa sababu hawana fedha ya kuwasomesha, hivyo mvuruge mvuruge majibu ili msifaulu.

“Nchi hii inataka watu wasomi, mwezi wa kwanza nitawapeleka bungeni Mjini Dodoma serikali ya chama cha mapinduzi inayoongozwa na Rais Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan imetangaza elimu bure ya msingi na sekondari hakuna ada,” alisema Waziri.

Dunia ya leo inahitaji watu wenye maarifa, tunasoma kwa ajili ya kuondoa ujinga niwaombeni wazazi muache watoto wasome. 

Naye Mwalimu Yasinta Chipanjile wa shule ya Msingi Iramba amesema amepata changamoto katika kipindi cha miaka miwili kutokana na kushindwa kucheza na akili za wazazi.

“Tunakwenda vizuri mitihani ya kata, mitihani ya ujirani mwema lakini kwenye mitihani ya kitaifa watoto hawafanyi vizuri kutokana na kikao cha kifamilia kinachofanyika wiki moja au siku mbili kabla ili kuwazuia watoto wasifaulu.”

Amefafanua alichukua sauti ya Waziri iliyotoa ari ya wanafunzi kufaulu kuanzia watoto 30 ili waweze kutembelea bunge, na kutembea na kauli hiyo Mpaka wakati wa mtihani yao ya kitaifa.

“Katika ufaulu huo wavulana walikuwa 12 na wasichana 20 ufaulu ambao haujawahi kutokea tangu shule ya msingi iramba ianzishwe, kutokana na shinikizo la wazazi kwa  watoto kutengeneza matokeo ya E .” Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa hadhara kijiji cha Iramba.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi washule ya msingi Iramba.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi katika kijiji cha Itamba.

Post a Comment

Previous Post Next Post