Watumishi wa Mahakama za Wilaya mpya nchini zilizozinduliwa hivi karibuni wanaendelea kupatiwa Mafunzo ya Huduma kwa mteja longo likiwa ni kuboresha utendaji kazi katika Mahakama hizo ili wananchi waweze kupata huduma bora ya utoaji haki.
Tarehe 25 Novemba, 2022 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alizindua Mahakama ya Wilaya Busega iliyowakilisha Mahakama nyingine mpya za Wilaya mpya 17, Mahakama hizo zilizojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia ni pamoja na; Butiama, Rorya, Songwe, Gairo, Mkinga, Mvomero, Kilombero, Mbogwe, Nyang’hwale, Kyerwa, Itilima, Missenyi, Kaliua, Uvinza, Buhingwe, Kakonko na Tanganyika.
Katika siku ya tatu ya Mafunzo hayo; Mada zilizotolewa ni pamoja na; Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania na ya Mabadiliko ya kiutendaji (Change Management).
Yafuatayo ni matukio katika picha ya Watoa mada mbalimbali waliotoa mada siku ya tatu (3) ya mafunzo hayo:-
Muonekano wa sehemu ya wasilisho la Mpango Mkakati lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso (hayupo katika picha).
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo wakifuatili mada inayotolewa.
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Andrew Msami akiendelea kuwasilisha mada, amewasisitiza watumishi kuwa chanzo cha mabadiliko kwa kuwa na mtazamo chanya (positive attitude) ili kuweza kufanya kazi zitakazoleta matokeo chanya.