MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI AMETEMBELEA VITUO VYA KUPIGIA KURA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA AMANI

 


  

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 17 Disememba, 2022, ametembelea na kukagua zoezi la upigaji wa kura kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Amani Tanzania Zanibar.

Jaji Mwambegele ameridhishwa na maandalizi ya vituo, kufunguliwa kwa vituo na ulinzi wa vituo. Vituo vimefunguliwa saa 01:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni. Uchaguzi huo unafanyika sambamba na kata saba (7) za Tanzania Bara.

Post a Comment

Previous Post Next Post