MATUKIO YA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIANCHI MISRI

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliotembelea banda la maonesho la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri. Wengine pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama, wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi akitoa ufafanuzi kwa wageni waliotembelea banda la banda la maonesho la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Post a Comment

Previous Post Next Post