Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumvusho ya MajiMaji Bi Rose Kingwe akitumia kishikwambi kutoa elimu ya utalii.
……………………..
Na Mwandishi wetu, Iringa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameipongeza Makumbusho ya Taifa, kwa kutoa elimu ya utalii kidigital.
Mhe. Waziri alizitoa pongezi hizo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Utalii yajukanayo kama Karibu Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Kihesa Mkoani Iringa.
Vile vile ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuendelea kuhifadhi historia adhimu ya vita vya MajiMaji ambapo kuna Makumbusho maalum ya kumbukizi ya vita hivyo mjini Songea.
“Naipongeza sana Makumbusho ya Taifa la Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi historia adhimu ya nchi yetu na kuitangaza kidigital” amesema Mhe. Waziri.
Maonesho hayo yamewaleta pamoja wadau mbalimbali wa masuala ya utalii kwa ajili ya kutoa elimu na kuhamasisha utalii nchini