Wataalamu
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mtwara pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Lindi – Sokoine watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa watoto na
watu wazima.
Mkoani
Mtwara upimaji utafanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Novemba, 2022
kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika viwanja
vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mtwara. Kwa taarifa zaidi kuhusu
upimaji utakaofanyika mkoani Mtwara wasiliana kwa namba 0685921947 Dkt.
Maximilliana Mwenda na 0686732326 Bi. Eshe Mnyanga.
Tarehe
2 hadi 4 Desemba, 2022 upimaji na matibabu ya moyo utafanyika mkoani
Lindi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine
kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni. Kwa taarifa
zaidi kuhusu upimaji utakaofanyika mkoani Lindi wasiliana kwa namba
0786066182 Dkt.Godwin Macheku na 0653134711 Dkt. Martin Kazi.
Tutakuwa
na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa
wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia
kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza
na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika
kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa
matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.
Tunawaomba
wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo
ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayebainika kuwa mgonjwa.