BoT KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI NCHINI- PROF. LUOGA

 

Gavana wa Benki Kuu ya tanzania (BoT) Prof. Florence Luoga akizungumza alipokuwa katika Mkutano wa siku mbili wa mawasilisho ya mada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maafali ya kwanza ya Chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25, mwaka huu.

Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu Dkt. Nicas Yabu akizungumza alipokuwa akitoa salamu za ukaribisho kwa wageni waliofika kwenye mkutano huo.

Picha za washiriki wa mkutano huo.

MWANZA.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florence Luoga amesema kuwa Benki hiyo imeendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha mfumuko wa bei haukui na kuleta athari za kiuchumi kwa Taifa.

Prof. Luoga ameyasema hayo Novemba 22,2022 katika Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza wakati wa mahojiano na waandishi wa habari katika Mkutano wa siku mbili wa mawasilisho ya mada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maafali ya kwanza ya Chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25, mwaka huu.

Amesema kuwa mfumuko wa bei Tanzania bado ni mdogo ambao ni asilimia 4.8 ikilinganishwa na nchi nyingine za Bara la Afrika na Ulaya ambazo hivi sasa zinakaribia asilimia 10 na zaidi na kwamba Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti mfumuko wa bei kutokana na wataamu wake kufanyakazi kwa weledi kuhakikisha kunakuwepo na udhibiti wa viashiria vitakavyosababisha kuwepo kwa athari hiyo.

“Kwa Tanzania kuwa na mfumuko wa asilimia 4.8 hiyo sio bahati bali imetokana na wataalamu wetu wanavyoweza kuangalia viashiria vya mfumuko wa bei kuongezeka ghafla na kuchukua hatua ya kuhakikisha mfumuko wa bei hautokei kwa ghafla hiyo.  Kwa hiyo kuna hatua maalum ambazo sisi tunazichukuwa Ili kuilinda nchi dhidi ya mfumuko wa bei” amesema Profesa Luoga.

Aidha amesema kuwa Tanzania imeendelea kuimarika katika sekta ya mambenki ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kwamba hatua hiyo  imetokana na uwepo wa waatalamu wa uendeeshaji katika Sekta hiyo.

Hata hivyo amesema kuwa kuimarika kwa Sekta ya Benki hapa nchini kunatokana na usimamizi mzuri wa Benki Kuu ambayo ndio muangalizi Mkuu wa Sekta hiyo na kuifanya iweze kuchagiza katika ukuaji wa uchumi. 

katika hatua nyinge Prof. Luoga amezungumzia umuhimu wa wataalamu wa Sekta ya fedha kuendelea kufanya utafiti ili kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta hiyo ambapo amezungumzia umuhimu wa uwepo wa Chuo cha Benki Kuu kilichojikita katika kuhakikisha kinazalisha wataalamu watakaokwenda Kusimamia Sekta ya Benki.

“Chuo chetu kimejikita katika kuhakikisha Sekta ya mabenki inapata wataalamu ambao watasimamia Sekta hiyo”

“Chuo chetu Kwa kushirikiana na vyuo vingine nchini vinaweza kuelekeza nguvu na juhudi za kufanya utafiti katika eneo zima la usimamizi wa Sekta ya fedha nchini”  

Hii ni Sekta ambayo inasimamiwa na Benki Kuu na ndiye mshauri Mkuu wa Serikali, ndio maana katika eneo zima la usimamizi wa Sekta ya fedha Benki Kuu lazima iwe huru kwa kushirikiana na wataalamu ambao inawategemea  kuhakikisha kuwa utafiti unafanyika na ufumbuzi unapatikana kabla athari hazijatokeza. Ndicho kitu tunachokifanya leo kuangalia tumefikia wapi katika kutayarisha wataalamu, tumefikia wapi katika kufanya utafiti, kwa kushirikiaha na wataalamu kutoka katika Taasisi nyingine kuhakikisha kuwa tunakuwa na uwezo katika kufanya utafiti kupata ufumbuzi na kutekeleza” amesema Prof. Luoga.

Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania kitafanya Maafali yake ya kwanza Ijumaa Novemba 25, 2022 toka kuanzishwa kwake na kuwa na jumla ya wahitimu 36 waliofanya vizuri na kufaulu masomo yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post