Mwezeshaji
wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu Uandaaji wa Bajeti kwa
Mrengo wa Kijinsia kwa maafisa mipango na bajeti, maendeleo ya jamii na
waratibu wa madawati ya jinsia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Jiji la Dar
es Salaam, wawakilishi kutoka ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Halmshauri za wilaya ya Kishapu, Mbeya, Kasulu,
Morogoro, Tarime, Same, Muheza na Moshi. Kwa Dar es salaam kuna
washiriki kutoka manispaa za ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke.
Afisa
Programu Idara ya Mafunzo kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),
Anna Sangai akizungumza kuhusu namna Mtandao huo unavyofanya kazi na
jamii hasa kwenye uandaaji wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia wakati wa
warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa
Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa
nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini
Dar es Salaam.
Mhadhili
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Lihoya Chamwali akitoa mada kuhusu namna
wanavyoweza kuweka usawa wakjinsia pamoja na kuweka bajeti yenye mlengo
wa kijinsia kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa
Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na
Madiwani kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini leo tarehe
Novemba 22, 2022.
Baadhi
ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya
Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini wakichangia
mada kwenye warsha ya kuwajengea uwezo kuhusu Bajeti yenye mlengo wa
jinsia inayofanyika kwa siku nne jijini Dar es Salaam.