MANDONGA MTU KAZI SASA 'RASMI'


Afisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), Bw. Goodluck Mushi (mwenye tai)akimpatia usaidizi wa usajili wa Jina la Biashara, Karim Mandonga, akipofika ofisi za BRELA tarehe 15 Novemba, 2022  kupata huduma na kusajili Jina la Biashara, Mandonga Entertainment.
Karim Mandonga (kulia) akikabidhiwa cheti cha Usajili wa Jina la Biashara na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Roida Andusamile,  katika ofisi za BRELA, mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili mapema  tarehe  15, Novemba, 2022 jijini Dar es Salaam.

                ...........................................
 Mwanamasumbwi ambaye amejipatia umaarufu katika siku za hivi karibuni, Bw. Karim  Halid Mandonga , maarufu kwa jina la Mandonga Mtu Kazi, hatimaye amesajili jina la Biashara  katika ofisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), baada ya kukamilisha taratibu za Usajili.

Akizungumzia hatua aliyofikia baada ya kukabidhiwa cheti cha Usajili wa jina la Biashara  Mandonga Entertainment tarehe 15 Novemba, 2022 Bw. Mandonga amesema, inatokana na jitihada  zilizofanywa na  uongozi wa BRELA za kumhamashisha  kusajili Jina la Biashara ambalo anaamini litamwezesha kufanya kazi zake bila ya kuwa na changamoto zozote.

Mandonga amesema kwa sasa yeye ni balozi wa BRELA  na ataendelea kuwahamasisha wanamichezo wengine kurasimisha biashara zao kwani michezo ni biashara.

"Nimefurahi sana kupata cheti hiki kwani kitanipa ulinzi wa kisheria na biashara zangu zitakwenda vizuri", amefafanua Bw. Mandonga.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA  Bw.  Godfrey Nyaisa akizingumza na Bw. Mandonga ofisini kwake amemtaka  kutokukubali kutumika kirahisi na watu wenye nia ya kujinufaisha wao wenyewe.

Bw. Nyaisa amemsihi  kuwasiliana na  BRELA muda wowote kwa ushauri wa kibiashara ili kutimiza ndoto zake.

Post a Comment

Previous Post Next Post