MHE. MCHENGERWA - CAF KUZINDUA “AFRIKA SUPER CUP

Na John Mapepele- Arusha

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Omary Mchengerwa amesema Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) unaofanyika kesho Agosti 10,2022 jijini Arusha Tanzania, unakwenda kuzindua mashindano maalum ya kandanda ya Afrika Super CUP.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Arusha leo, Agosti 9, 2022 Mhe. Mchengerwa amesema mkutano huo ambao ni wa kwanza wa kihistoria katika Bara la Afrika na Tanzania unafaida kubwa kiuchumi na kimichezo. 

Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa baadhi ya wageni wanaoshiriki kwenye mkutano huo wameshapanga kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii hapa nchini baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

Mchengerwa amesema mkutano huo wa 44 unatarajiwa kufanyika kesho ambapo unajumuisha mataifa 58 na nchi 54 ni za Afrika.

Aidha, amesema ni nchi mbili tu za Afrika yaani Kenya na Zimbabwe ambazo zinatumikia adhabu ambazo hazishiriki kwenye mkutano huo.

Amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe na Rais wa FIFA Gianni Infantino ambapo pia Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa atamwakilisha Rais. Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha zaidi ya watu mia tano aambapo zaidi  ya wandishi wa habari mia moja wa ndani na nje ya Tanzania wanatahudhuria na kuangaliwa mbashara na zaidi ya watu bilioni moja duniani kote.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post