Na John Mapepele, Arusha
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku huu ameongoza ujumbe wa kumpokea Rais wa FIFA Gianni Infantino anayekuja kuhudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Mkutano huo wa kwanza wa kihistoria unafanyika kwa mara ya kwanza nchini huku zaidi ya nchi 58 kutoka sehemu mbalimbali duniani zikishiriki.
Mhe. Mchengerwa amemkaribisha Rais wa FIFA Gianni na kumpatia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumwelezea jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ambapo Rais wa FIFA ameelezwa kuridhishwa na maendeleo ya Michezo.
Amepongeza kazi kubwa huku akisema amefurahishwa na makaribisho hayo.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na kuangaliwa na watu zaidi ya bilioni moja.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Mhe. Rais.
Katika mkutano huo CAF inakwenda kuzindua mashindano maalum ya soka ya soka ya Afrika Super CUP