DKT. PINDI CHANA: WATANZANIA TEMBELEENI VIVUTIO VYA UTALII

 


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi chana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea banda la Wizara hiyo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi zilizopo kwenye Wizara hiyo.

Watumishi wa Bodi ya Utalii wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao mara baada ya kutembelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii dkt. Pindi Chana leo Julai 11,2022 katika maonesho ya sabasaba jijini dar es salaam.

Na: Mwandishi wetu, DSM

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana amewahimiza watanzani na wananchi wote kwa ujumla kujenga utamaduni wa kutembelea katika maeneo mbalimbali ya utalii ili kujifunza na kukuza utalii wa ndani.

Amesema kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo muhimu ambalo Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo na kuhamasisha watanzani kujenga utamaduni wa kufanya utalii wa ndani.

Waziri Chana ameyasema hayo leo Julai 11,2022 katika Banda la Wizara yake kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar ea salaam na kufanya ziara ya kutembelea Taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara hiyo ambapo amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hizo.

Amesema kuwa Sekta ya Utalii imeendelea kukua kwa kasi kubwa na imekuwa ikichangia kwa asilimia 17 katika pato la Taifa sambamba na kutoa ajira kwenye maeneo mbalimbali katika sekata hiyo ambazo watanzania wamenufaika katika ajira hiyo.

“Niwaombe watanzania na wananchi wote kwa ujumla kutembelea Banda hili la Maliaasili na Utalii ili kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi zetu zilizopo hapa na kufahamu shughuli wanazofanya na kufurahia huduma wanazozitoa ndani ya maonesho haya. ” amesema Waziri Chana.

Kwa upande wao Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema kuwa katika moja ya shughuli wanazozifanya katika maonesho hayo ni pamoja na kuwahamasisha wananchi wote kuanzisha vikundi vya utalii wa kiutamaduni unaolenga kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mila na tamaduni mbalimbali za makabila ya kitanzania.

Akizungumza katika mahojiano maalum mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Waziri wa Maliasili Dkt. Pindi Chana, Afisa Habari wa TTB Agustina Makoye amesema kwa sasa Bodi hiyo imeanza kutoa hamasa taratibu kutokana na makabila mengi kukosa uelewa wa kutangaza vitu walivyonavyo.

“Kama Bodi ya Utalii tayari tumeanza kuhamasisha na kuwafundisha wananchi katika maeneo mbalimbali namna ya kuvielezea vivutio vyao ikiwemo vitu vya asili kama maporomoko ya maji, vyakula pamoja na vitu mbalimbali na vivutio vinavyopatikana kwenye maeneo yao” amesema Agustina.

Ametoa mwito kwa wananchi kuhamasika katika kufanya utalii wa ndani na kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia kutangaza vivutio vilivyopo katika maeneo tofauti nchini.


Post a Comment

Previous Post Next Post