UJENZI WA KIWANDA CHA KUWEKA PLASTIKI KATIKA MABOMBA YA KUSAFIRISHA MAFUTA WAANZA

 

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, akizungumza na vyombo vya habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda cha kuweka plastiki ili kuzuia kutu kwenye mabomba yakusafirisha mafuta ghafi, na kupasha moto mafuta hayo katika mradi wa bomba kusafirisha mafuta( EACOP), kilichopo katika eneo la Sojo, wilayani Ngega Mkoani Tabora

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, akizungumza na vyombo vya habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda cha kuweka plastiki ili kuzuia kutu kwenye mabomba yakusafirisha mafuta ghafi, na kupasha moto mafuta hayo katika mradi wa bomba kusafirisha mafuta( EACOP), kilichopo katika eneo la Sojo, wilayani Ngega Mkoani Tabora,

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba,(pili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, ( katikati), Msimamizi wa Mradi huo Kitaifa, Wizara ya Nishati Kisamarwa Nyang’au, na Mkuu wa Wilaya ya Nzega (ACP) Advera Bulimba, wakijadiliana mambo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda cha kuweka plastiki ili kuzuia kutu kwenye mabomba yakusafirisha mafuta ghafi, na kupasha moto mafuta hayo katika mradi wa bomba kusafirisha mafuta( EACOP), kilichopo katika eneo la Sojo, wilayani Ngega Mkoani Tabora, Julai 7, 2022.

Msimamizi wa Mradi huo Kitaifa, Wizara ya Nishati Kisamarwa Nyang’au, (kulia) akizungumza na vyombo vya habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda cha kuweka plastiki ili kuzuia kutu kwenye mabomba yakusafirisha mafuta ghafi, na kupasha moto mafuta hayo katika mradi wa bomba kusafirisha mafuta( EACOP), kilichopo katika eneo la Sojo, wilayani Ngega Mkoani Tabora, Julai 7, 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba,(katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, wakiwa katika picha ya pamoja na wasimamizi wa mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha kuweka plastiki ili kuzuia kutu kwenye mabomba yakusafirisha mafuta ghafi, na kupasha moto mafuta hayo katika mradi wa bomba kusafirisha mafuta( EACOP), wakati wa ziara ya kukagua kiwanda hicho kilichopo katika eneo la Sojo, wilayani Ngega Mkoani Tabora, Julai 7, 2022

……………….

Na Zuena Msuya, Tabora

Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba wamewataka watanzania kuchangamkia fursa zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongolieani mkoani Tanga, (EACOP).

Makatibu Wakuu hao walisema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda cha kuweka plastiki ili kuzuia kutu kwenye mabomba yakusafirisha mafuta ghafi, na kupasha moto mafuta hayo katika mradi wa bomba kusafirisha mafuta( EACOP), kilichopo katika eneo la Sojo, wilayani Ngega Mkoani Tabora, Julai 7, 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema kuwa katika kutekeleza mradi huo mkubwa unaohusisha nchi mbili Tanzania ya Uganda, tayari kiwanda hicho kuweka plastiki ili kuzuia kutu katika mabomba ya chuma yatakayotumika kusafirisha mafuta umeanza.

Mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho, Shehena ya Kwanza ya Mabomba inatarajiwa kuingia nchini mwanzoni mwa mwaka 2023 na Ujenzi utachukua Miaka 3, kuanzia sasa.

Pamoja na mambo mengine amewataka watazania kuchangamkoa fursa za ajira pamoja na kufanya shughuli za kibiashara katika kila eneo ambalo kazi za awali za utekelezaji mradi huo zinafanyika ili kujiongezea kipato kwa kunufaika na uwepo wa mradi huo.

Aliweka wazi kuwa Katika kutekeleza mradi huo wa kiwanda, mkataba wa dhana ya ushirikishwaji wa jamii katika mradi huo ulizingatiwa ambapo liwekwa bayana kuwa Kazi za ujenzi, Vyakula na Vinywaji, Malazi, usafiri, ulinzi zitatolewa na Wazawa.

“Watanzania changamkieni fursa anzisheni biashara mbalimbali, kulingana na uhitaji ikiwemo vyakula, kupata zabuni ya kusambaza vifaa vya ujenzi na kuomba kazi za ujenzi kwa wale wenye makampuni sababu kazi hiyo inafanywa na Watanzania, kama mkataba unavyolekeza, kila mmoja ajivunie na anufaike na mradi huo”, alisisitiza Mhandisi Mramba.

Alisema kazi kubwa itayofanyika sasa baada ya kiwanda hicho kukamilika uunganishaji wa vipande vya bomba ili kupata bomba moja refu, hivyo mafundi wa uchomeleaji wa chuma watahitajika kwa wingi na watakaobahatika waonyeshe uwezo wao na kuifanya kazi hiyo kwa weledi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba, amesema Serikali ya Tanzania imewekeza hisa asilimia 15 kwenye mradi huo ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya Trilioni 11, hadi kukamilika kwake.

Anasema katika mradi huo, tayari Serikali ya Tanzania imeshatoa fedha Taslimu ambazo ni sawa na asilimia 40 ya fedha zake katika mradi huo na sababu ya wao kufanya ziara ili kuona maendeleo ya utekelezaji wake.

“Kwenye mradi huu wa bomba la mafuta Serikali ya Tanzania tuna Hisa asilimia 15 na tayari tumeshatoa kiasi cha fedha, na ndiyo maana tunafuatilia ili kuona maendeleo ya ujenzi wa mradi huu, Natoa wito kwa Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa za ajira kwenye mradi huu wa bomba la mafuta, ambao unafaida kubwa kwa Watanzania kiuchumi,” amesema Tutuba

Alisema Kwa mujibu wa Mkataba wa utwaaji wa Ardhi kwa ajili ya Mradi wa EACOP Sheria za ndani ya Nchi ulitumika ili kuruhusu Kampuni ya EACOP kuweza kukopesheka.

Aidha,

Serikali na Mradi wa EACOP zilikubaliana kuwa fedha za ulipaji fidia zitatolewa na Kampuni ya EACOP na gharama hiyo itakuwa sehemu ya gharama za mradi.

Utwaaji wa Ardhi ya mradi kwa Tanzania unafanyika katika Makundi Makuu matatu (3) ambayo ni Maeneo ya Kipaumbele ya Mradi, Maeneo ya Mkuza na Maeneo ya Bandari.

Utwaaji wa Ardhi katika maeneo hayo yenye ukubwa wa ekari 637.08 umekamilika ambapo jumla ya Wananchi 387 wamelipwa jumla ya shilingi bilioni 2.286.

Maeneo hayo yatakodishwa kwa EACOP kwa kipindi cha miaka mitano (5), ambapo Serikali inatarajia kukusanya jumla ya dola za marekani 289,000 (takriban shilingi milioni 664.7) kila mwaka kama pango la Ardhi katika maeneo hayo ya Kipaumbele.

Eneo la Mkuza wa Bomba kwa upande wa Tanzania lina urefu wa kilomita 1147 kutoka Mtukula – Misenyi hadi Chongoleani Tanga. Jumla ya Wananchi 9125 wanatarajiwa kulipa fidia ya jumla ya Shilingi Bilioni 22 ili kupisha maeneo hayo.

Aidha mradi huo pia unatarajia kutwa eneo la bahari yenye ukubwa wa ekari 72 kwa ajili ya matumizi.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi huo Kitaifa, kutoka Wizara ya Nishati Kisamarwa Nyang’au alisema kuwa kazi ya kwanza katika eneo la Kiwanda hicho lenye ukubwa wa lenye ukubwa wa ekari 98.7 ilikuwa ni kulipa fidia kwa wakazi wote wa eneo hilo ili kupisha eneo la mradi ambapo kila aliepisha mradi alipewa uhuru wa kuchagua namna bora kwake ya kulipwa fidia, kuwa ajengewe nyumba nyingine kulingana na idadi ya nyumba alizonazo ama alipwe fedha taslimu.

Katika Eneo la Kiwanda kulikuwa na Wananchi 34 ambao walilipwa fidia ya jumla ya shilingi milioni 269, Kati yao, Wananchi 9 walihamishwa kwa kubomolewa Makazi yao na kujengewa nyumba kulingana na idadi ya nyumba walizonazo, ambapo Nyumba 12 zilijengwa na kukabidhiwa Wananchi hao, na mwananchi mmoja alijengewa nyumba 4 kwa kuwa ndizo alizokuwa nazo kabla ya uwepo wa mradi.

Nyang’au alisema kuwa  wakazi hao wamejengewa nyumba za kisasa zenye idadi sawa ya vyumba na nyumba aliyonavyo kabla ya kupisha mradi, pia wamejengewa choo na jiko la nje , uwamekewa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa lita elfu 5( 5,000) pamoja na Umeme wa Jua(Solar)  wenye uwezo wa Watti 400.

Katika hatua nyingine amewatoa wasiwasi Watanzania, kuwa kwenye mradi huo wa bomba la mafuta hakutakuwa na uharibifu wowote wa Mazingira, bali wamejipanga vyema kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega (ACP) Advera Bulimba, amesema ujenzi wa kiwanda hicho upo salama, na hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi, huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kupeleka ujenzi wa kiwanda hicho wilayani humo ambapo wananchi wake wananufaika nao kiuchumi.

Nao baadhi ya wananchi wa eneo hilo la Mradi wa Bomba la Mafuta akiwamo Magimbi Nagaja, anasema yeye ni miongoni wa watu ambao wamefidiwa kupisha mradi huo na amejengewa nyumba nzuri na sasa anafanya tena kazi za kibarua na kumuingizia kipato

Post a Comment

Previous Post Next Post