SHIRIKA LA MADINI STAMICO LATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA MOI

 


Wafanyakazi wa Shirika la Madini STAMICO  wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali yenye thamani ya shilingi ilioni 2.2 Kwa watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) ikiwa na lengo la kusaidia mahitaji Kwa watoto hao wagonjwa.

Mbali na Msaada huo Shirika hili pia limechangia gharama ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya  matibabu ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa katika taasisi hiyo.

Akielezea zaidi kuhusu msaada huo Biniana Ndumbaro amesema wamefanya hivyo katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma ili kuchangia kidogo kilichopo kwa ajili ya kutatua changamoto ya magonjwa vichwa vikubwa inayokabili baadhi ya watoto kwenye jamii ambapo jumla ya msaada huo ni shilingi milioni 4.2.

Afisa Habari wa Shirika hilo Bi. Bibiana Ndumbaro akimjulia hali mmoja wa watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipotoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa watoto hao wagonjwa.

Wafanyakazi wa Shirika la Madini STAMICO wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali yenye thamani ya shilingi ilioni 2.2 Kwa watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) ikiwa na lengo la kusaidia mahitaji Kwa watoto hao wagonjwa kulia ni Theresia Jacob Afisa Maendeleo na Elimu kwa watu wazima (MOI)

Theresia Jacob Afisa Maendeleo na Elimu kwa watu wazima (MOI) akitoa maelezo kwa baadhi ya wafanyakazzi wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO walipokwenda kutoa msaada wa mahitajimbalimbali kwa watoto wenye matatizo ya Vichwa Vikubwa na Mgongo wazi waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI)

 

Mafanyakazi wa Shirika la Madini STAMICO Mhandisi Pili Athumani  wakigawa vitu mbalimbali kwa watoto waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa ya MOI jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post