TRA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WACHINA WAWILI, ZHU WEI NA TAO PAN

Leo tarehe 15/6/2022 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikisha watuhumiwa wawili Raia wa China Bw. Zhu Wei na Bw. Tao Pan  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa makosa ya kukutwa na bidhaa ambazo hazijafuata taratibu za forodha,  kukwepa kodi na uhujumu uchumi. Mashtaka hayo yamesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Rita Tarimo ambaye ameiahirisha kesi hiyo  hadi tarehe 29/6/2022.



 

Post a Comment

Previous Post Next Post