Katika maonesho haya JKCI inafanya upimaji wa afya ya moyo kwa watoto na watu wazima. Pia inatoa chanjo ya UVIKO-19 kama kinga ya ugonjwa huu pamoja na kufanya kipimo cha kuchunguza UVIKO -19 (rapid test) kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo katika njia ya kupumulia.
Taasisi hiyo pia ina wataalamu wa lishe ambao wanatoa elimu ya lishe bora ambayo inawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo na kisukari ambayo ni magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu wa lishe.
Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu hii ikiwa ni pamoja na kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.
Madaktari mabingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI ya kina Peter Kisenge, Tulizo Shem, Tatizo Waane, Baraka Ndelwa na Pedro Pallangyo chini ya uongozi wa Prof. Mohamed Janabi watakuwepo katika banda letu kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Nyote mnakaribishwa