NAOGOPA SANA WATU WANAORIDHIKA KWENYE ELIMU

 Na Mwandishi wetu Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa anaogopa sana watu wanaoridhika kwenye elimu kwa kudhani kuwa wamefika wakati bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha elimu yetu inaboreshwa.

Prof. Mkenda alibainisha hayo leo Juni 13,2022 alipokuwa akifunga maonyesho ya Elimu ya sayansi na mafunzo ya ufundi stadi yaliyofanyika jijini Dodoma.

Amesema kuwa kama elimu yetu ni bora basi kusingekuewa na ulazima kwa baadhi ya makampuni kuajiri watu kutoka nje ya nchi hivyo kwa maana hiyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha elimu yetu inakidhi mahitaji yanayotakiwa katika soko la ajira.

"Lazima tukubali kuwa elimu yetu bado na inahitaji tuendelee kufanya kazi kwa nguvu sana ili kuiboresha kwa sababu ukweli ni kwamba kuna vyuo mpaka sasa vinatoa wanafunzi ambao baada ya kumaliza mafunzo hawaajiri kabisa kutokana na kutokuwa na ubora hivyo ndugu zangu tusiridhike hatujafika kabisa",Amesema Prof.Mkenda

Pia Prof.Mkenda amegusia jitihada ambazo serikali inaendelea kufanya ni kutafuta mikopo na benk ya NMB imekubali kutoa sh. bilion 200 kwa ajili ya kukopesha wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati na ufundi nchini.

“Mikopo hii haitakuwakama ile inayotolewa na Bodi ya Mikopo kwahiyo kama ni mfanyakazi atahitaji kumsomesha mtoto wake VETA atapewa mkopo huo kwa masharti nafuu,”alisema.

Profesa Mkenda amesema katika kuhakikisha zoezi la kutoa mikopo katika ngazi hiyo linakuwa kwa ufasaha inahitajika kuwa na takwimu mahusus za vyuo vyote vinavyotoa mafunzo.

“Tukiwa na takwimu sahihi tukajua ni kozi gani ambazo wanafunzi wakisoma wanaajiriwa haraka tunaweza kuongea na benk zetu wakatoa mikopo kwa wanafunzi hao na watarejesha wenyewe pindi watakapo ajiriwa au kujiajiri hii itasaidia kupanua wigo wa wanafunzi wanaomaliza vyuo na kujiajiri au kuajiriwa,”ameleza

Amewaagiza Baraza la Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya UFUNDI Stadi (NACTVET) kuhakikisha wanasimamia maudhui yanayotolewa katika vyuo ili kuendelea kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan alityoyatoa wakati akihutuba bunge.

“Rais Samia wakati akihutubia bunge aliagiza wizara ya Elimu kupitia sera na mitaala ya elimu ili kuongeza ubora wa elimu kuhakikisha elimu inayotolewa inaleta ujuzi ilikumuandaa muhitimu kumudu mazingira ili aweze kuajirika na kujiajiri,”alisema.

Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa NACTVET Dk. Adolf Rutayuga alisema katika kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa elimu ya mafunzo stadi yenye ubora zaidi hadi kufikia juni 2022 baraza lilikuwa limesajiri vyuo 454 vya elimu ya ufundi.

alisema kati ya vyuo 454 vyuo 179 ni vya serikali na vyuo 275 ni vya sekta binafsi.

“Idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo imeongezeka kutoka 1,17474 katika mwaka wa masomo 2014/2015 hadi kufikia 2,10775 mwaka 2020/2021 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi wengi zaidi hasa katika vyuo vya sekta binafsi ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa,”alisema.


 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof Adolf Mkenda akizungumza leo Jijini Dodoma wakati  akifunga  maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi yalihitimishwa  Katika uwanja wa Jamhuri.

Post a Comment

Previous Post Next Post