TIC YAKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA UVUVI MWANZA KUKUSANYA MAONI KUHUSU MAZINGIRA YA UWEKEZAJI

 


Mafutah Bunini Mkurugenzi wa utafiti wa mipango na mifumo ya taarifa kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania TIC akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi .
Meck Sadiki Mkurugenzi wa Kampuni ya Sameki inayojihusha na ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba akizungumza na waandishi wa habari namna ambavyo Serikali imewafitia baadhi ya kodi katika shughuli zao.
Girson Ntimba Meneja wa kituo cha uwekezaji Kanda ya ziwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano.
Wadau wa Sekta ya uvuvi wakiwa kwenye Mkutano 
………………………………………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya ziwa kimefanya mkutano na wadau wa sekta ya uvuvi kwa lengo la kukusanya na mapendekezo kuhusu mazingira ya Uwekezaji katika sekta hiyo.
Mkutano huo umefanyika leo Alhamisi Juni 23,2022 katika ukumbi wa Gold crest uliopo Jijini Mwanza.
Akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), Mkurugenzi wa utafiti mipango na mifumo ya taarifa kutoka  kwenye kituo hicho Mafutah Bunini,amesema Sekta ya uvuvi ni muhimu katika nchi kwani inawezesha kuboresha afya za watanzania kupitia samaki ambao wanaongeza protini mwilini na inamchango mkubwa kwenye kuchangia pato la Taifa.
“kwamujibu wa taarifa ya hali halisi ya uchumi inayotolewa na kituo cha takwimu (NBS) mwaka 2020 sekta hii imechangia pato la Taifa kwa asilimia 1.8”,amesema Bunini
Ameeleza kuwa pamoja na umuhimu huo kumekuwepo na changamoto zinazoikabili sekta ya uvuvi hali ambayo inasababisha sekta hiyo kushindwa kufikia malengo yake.
“Sisi kama kituo cha uwekezaji tukaona tufanye mkutano na wadau hawa ili kwapamoja tujadiliane hali halisi ya uwekezaji na mwisho tushauriane nini kifanyike ili kuweza kuboresha utendaji wa sekta hiyo hali itakayosaidia Pato la taifa kuongezeka”,ameeleza Bunini
Ameongeza kuwa takwimu zinaonyesha Tanzania ni nchi ambayo imezungukwa na maziwa,bahari na mito hivyo tunauwezo wa kuzalisha takribani tani milioni 3.2 za mazao ya samaki kama tukiyatumia ipasavyo,lakini kutokana na uzalishaji ambao umekuwa ukifanya kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya mifugo na uvuvi ya mwaka 2019 bado tunazalisha chini ya tani 1.
Bunini amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho wamesajili miradi ya sekta ya uvuvi 165 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 588 na kutoa ajira elfu 25,269 hivyo Uwekezaji katika sekta hii ni muhimu sana kwa wananchi na ukuaji wa kiuchumi.
Kwa upande wake Meneja wa kituo cha uwekezaji Kanda ya ziwa Girson Ntimba,amesema   mkutano huo ni muhimu sana hasa kwa upande wa Kanda ya ziwa ambapo wanatengeneza fursa za Uwekezaji kwa kuvutia zaidi wawekezaji kuleta mitaji kutoka nje na ndani ya nchi kwa lengo la kuwekeza kwenye Viwanda vya samaki.
“Takwimu zinaonyesha kwamba bado ziwa Victoria hatujalitumia vizuri ipasavyo hivyo bado ni fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza kwenye Viwanda vya samaki katika Mikoa ya Kanda ya ziwa ili kuweza kuboresha maisha ya watanzania”,amesema Ntimba
Awali akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu Joachim Otaru, amekipongeza kituo cha uwekezaji kwa namna kinavyofanikisha Uwekezaji nchini hususani katika kanda ya ziwa huku akisema wataendelea kuunga juhudi za kituo hicho.
Amesema asilimia 53 ya Mkoa wa Mwanza ni maji na asilimia 47 ni ardhi sehemu kubwa ya ziwa Victoria haijatumiwa ipasavyo licha ya kuwepo na fursa nyingi ikiwemo ya ufugaji wa samaki,utalii na mnyororo wa thamani kwenye maji kwaajili ya uchumi wa bluu.
Naye mshiriki wa mkutano huo ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Sameki inayojihusha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba Meck Sadiki, ameushukuru Serikali kwa kuondoa baadhi ya Kodi ambazo zilikuwa zinawabana wafugaji hao ikiwemo ya Kodi ya chakula,nyavu na injini hali iliyosaidia wafugaji kufuga katika mazingira salama na rafiki.
Ameeleza kuwa pamoja na kuondoa kodi hizo bado wanakabiliana na changamoto ya gharama kubwa ya ununuzi wa chakula cha mifugo, hivyo ameiomba Serikali kuhamasisha wawekezaji hapa Nchini kutengeneza chakula chenye ubora unaotakiwa.
“Nilikuwa naagiza kontena ya chakula mchanganyiko Cha samaki kwa Dola elfu 28 hadi Dar es salaam lakini tangu vita ya Ukraine ilipotokea  sasa hivi gharama imepanda hadi Dola elfu 38”,ameeleza Sadiki

Post a Comment

Previous Post Next Post