Mhe. Mchengerwa atoa mambo 10 yanayoipaisha Tanzania duniani


Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania imeandika historia ya kuingia kwenye mafanikio makubwa ya kidunia kwenye sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezio katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja chini ya Rais Samia suluhu Hassan.

Akizungumza wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/23 ya Wizara yake bungeni leo,Juni 6, 2022. 

Mhe, Mchengerwa amesema kutokana na ufanisi uliooneshwa na Tanzania katika maandalizi ya mashindano ya urembo, utanashati na mitindo kwa Viziwi ngazi ya Afrika, Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kidunia yatakayofanyik Oktoba, 2022 mwaka huu Jijini Dar es Salaam. 

Aidha amesema katika kipindi hiki Kiswahili kilipitishwa kuwa Lugha ya Kazi ya Umoja wa Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika tarehe 5 - 6 Februari, 2022 Jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Ameongeza kuwa Timu ya Taifa ya Soka la Walemavu (Tembo Warriors), ilianzisha safari ya kwenye mashindano ya dunia ya soka baada ya Novemba, 2021 kufuzu kwenda kucheza Kombe la Dunia nchini Uturuki Oktoba, 2022.

Ameongeza kuwa timu ya Twiga Stars iliyotwaa Kombe la COSAFA mara tatu mfululizo na Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya U17 ya Serengeti Girls ambayo imefuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa Wanawake.


Wizara kwa kushirikiana na wadau iliandaa maonesho ya mechi ya fainali ya Kombe la Klabu bingwa Ulaya (UEFA) kati ya Timu ya Real Madrid na Liverpool iliyofanyika tarehe 28 Mei, 2022 ilioneshwa katika Daraja la Tanzanite Jijini Dar es Salaam na tukio hilo lilirushwa mubashara kwenye luninga kupitia king’amuzi cha Dstv ambapo Dunia nzima iliitazama Tanzania kupitia mechi hiyo.

Serikali katika kipindi hiki kwa mara ya kwanza imeridhia kutoa asilimia tano (5) ya kodi ya michezo ya kubashiri matokeo ya michezo kupitia BMT kama chanzo cha mapato katika Mfuko wa Maendeleo ya Michezo nchini ikiwa ni juhudi za kimkakati za kusaidia maendeleo ya michezo nchini.  

Wizara inaendelea na upanuzi wa miundombinu katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ambapo inajengwa Hosteli mpya na ya kisasa kwa ajili ya makazi ya wanachuo.

Amesema kazi kubwa ya kupigiwa mfano iliyoanza kufanyika ni kuanza kushughulikia tatizo sugu la miundombinu ya michezo ambayo kwa muda mrefu imekuwa na changamoto au kuanzisha miundombinu mipya inayoendana na matakwa ya sasa. Serikali imekamilisha uboreshaji wa mfumo wa usajili na utoaji wa Leseni kwa Watumiaji wa Kazi za Ubunifu kwa njia ya kielektroniki (AMIS) uliozinduliwa rasmi tarehe 22 Novemba, 2021.

Pia amesema katika kipindi hiki katika kuhakikisha haki za wasanii zinapiganiwa, utendaji na usimamizi wa COSOTA uliimarishwa na kuweka rekodi ya ukusanyaji wa mirabaha ambapo kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2021 hadi 31 Desemba, 2021 jumla ya Shilingi 312,290,259 zilikusanywa na kugawanywa kwa wasanii wa muziki ambapo jumla ya wanufaika 1,123 wenye kazi 5,924 walipata mirabaha.

Serikali imerejesha Tuzo za Muziki, kwa upande wa filamu, Serikali ya Awamu ya Sita, kupitia Bodi ya Filamu Tanzania imefanya mageuzi ya kukumbukwa kwa kuanzisha, kwa mara ya kwanza Tuzo za Kitaifa za Filamu.

 Aidha Wizara imeendelea kuandaa matukio makubwa na ya kimkakati ikiwemo Tamasha kubwa la Kitaifa la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival).


 

Post a Comment

Previous Post Next Post