STAMICO Yahamasisha Matumizi Ya Mkaa Mbadala Wa Rafiki Briquettes

 

Wafayakazi wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi Mkoa Wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Deusdedith Magala akizungumza na waandishi habari katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na bdhaa mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo.

*Ni katika Siku ya Wafanyakazi Mkoa Dar es Salaam yaahidi kwenda kasi katika kutoa huduma kwa Wananchi.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutumia mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) utokanao na madini ya makaa ya mawe ili kuchangia utunzaji wa uoto wa asili na kupunguza uharibifu wa mazingira na ukataji miti ovyo.

Kutokana na mabadiliko ya Tabianchi mkaa wa Briquettes unakwenda kutatua changamoto uhalibifu wa mazingira wa kukata kwa ajili ya matumizi ya majumbani na kupikia

Elimu hii imetolewa kupitia siku ya wafanyakazi Mei Mosi Mkoa wa Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika hilo Deusdedith Magala amesema wanaadhimisha maadhimisho wakiwa wana nguvu zaidi ya kutaka wananchi wachangamikie bidhaa hiyo.

Amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanaenda kufungua mwanga na mategemeo ya serikali katika kuboresha masilahi ya wafanyakazi kama kauli mbiu ya mwaka huu ililivyojikita.

Magala amesema kuwa STAMICO ina vitu vizuri wananchi wanaweza kwenda kupata elimu pamoja na wachimbaji wadogo wa madini kupata elimu na wale wanaotaka kuongia katika sekta hiyo.

Akiongea kuhusu mpango mkakati wa STAMICO katika kuutangaza mkaa huo amesema Shirika limedhamiria fursa yeyote ya mikusanyiko mbalimbali zinazojitokeza ili kufikisha elimu kuhusu Mkaa huu.

Magala amesema mkaa hu umeletwa ili kuleta tija kwa mazingira ya nchi yetu na utumiaji wa mkaa huu utapunguza kasi ya ukataji miti katika maeneo mengi ya nchi hivyo mkaa huu ni rafiki kwa mazingira, matumizi.

"Mkaa huu una tija sana kwa wananchi wote hasa wanaotumia nishati ya mkaa wa miti, hivyo ni vyema Shirika likajipanga kuzalisha kwa wingi na kuusambaza kwa wananchi"amesema Magala

Shirika linaendelea kutoa elimu ya mkaa wa Rafiki Briquette kupitia mikutano, makongamano mbalimbali ili kuchochea matumizi ya mkaa huo ambao umetengenezwa kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani,mashuleni na maeneo mengine yenye uhitaji wa nishati ya kupikia kama hii.

Post a Comment

Previous Post Next Post