BRELA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUACHA KUFANYA BIASHARA KWA MAZOEA


 NA FARIDA SAID.MORGORO. 

Wafanyabiashara nchini wametakiwa kuacha kufanya biashara kwa mazoea na badala yake wafuate sharia zilizopo ikiwa ni pamoja na kusajiri jina la biashara au kampuni ili kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya wafanyaiashara na wamiliki wa makampuni. 

Rai hiyo imetolewa  Mkoani Morogoro na Afisa Leseni kutoka Wakala wa Usajili  wa Bashara na Leseni BRELA Bi. Sweetness Madatu kwenye maonyesho ya tano ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Kwa upande wao wakazi wa Mkoa wa Morogoro waliotembelea banda la BREALA katika viwanja vya Jamhuri wameupongeza  Wakala huo kwa elimu wanayoitoa kwa wananchi hao  juu ya Umuhimu wa kusajili Bishara zao katika mamlaka hiyo.

Wakizungumza na Waandishi wa habari wakazi hao wamesema kuwa licha ya kusogezewa huduma kwa ukaribu zaidi hivi sasa wanantambua umuhimu wa kusajili biashara zao kwani itawasaidia kuondosha bughudha katika kuteleza majukumu yao ya kila kisu.

Aidha wamesema kupitia elimu inayotolewa na BRELA inawaongezea uelewa wa kutanua shughuri zao za biashara ndani na nje ya nchini kwani wamekuwa wakitambuliwa kimataifa kupitia majina ya biashara au kampuni zao.

Sanjari na hilo wamesema kuwa usajili wa biashara kwa njia ya mtandao imekuwa huduma rahisi kwani kunamuwezesha mteja kupata cheti chake papo kwa papo hasa kwa wale waishio vijijini na kuondoa usumbufu wa kuzifuata huduma za usajili katika ofisi za BREALA zilizopo Mjini.

Post a Comment

Previous Post Next Post