Mhe. Mchengerwa atoa neno siku ya Utamaduni wa vyakula vya asili vya Uturuki

Na John Mapepele.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Mei 26, 2022  amehudhuria  kilele cha siku ya Utamaduni wa vyakula vya asili vya Uturuki kwenye ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam pamoja na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Uturuki kwenye sekta za Utamaduni na Sanaa kwa faida ya nchi zote mbili.

Mhe. Mchengerwa amesema ameishukuru Serikali ya Uturuki kwa kujenga kituo cha utamaduni hapa nchini.

Amesema Tanzania itaendeleza  ushirikiano huo kwenye sekta ya Utamaduni ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika eneo la wataalam wa Utamaduni.

Aidha amepongeza Uturuki kuendelea kutangaza lugha ya kiswahili duniani kupitia filamu zao zinazotafriwa kwa lugha ya kiswahili.

Ameongeza kuwa mwaka huu, Tanzania inakwenda kuadhimisha siku ya kiswahili duniani kuanzia Julai mosi hadi kilele chake Julai saba  kwa kufanya program mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya maonesho ya mapishi ya vyakula vya asili kutoka kwenye mbalimbali nchini. 


Waziri Mchengerwa ameiarika Uturuki  kushiriki kwenye maadhimisho ya siku hiyo kwa kuonesha vyakula  asili vya nchi hiyo kama ambavyo mataifa mbalimbali yatakavyoshiriki.

Naye Balozi wa Uturuki nchini. Mhe, Dkt. Mehmet Gulluoglu amesema ameishukuru Serikali ya Tanzania na kuahidi ushirikiano kwenye sekta za Utamaduni na Sanaa kwa faida ya nchi zote mbili.

Hafla hiyo imepambwa na msanii Godfrey Kapandila ambaye alitoa burudani ya nyimbo kadhaa ikiwemo malaika.



 

Post a Comment

Previous Post Next Post