TRA Pwani yakamata Magendo Bagamoyo

Mwandishi Wetu,

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imekamata magendo ya bidhaa katika Wilaya ya Bagamoyo ikiwemo viroba 50 vya mchele, madumu 10 ya mafuta ya kula na sabuni box 25 Aina ya Malaika.

Magendo hayo yalikamatwa kufuatia operesheni ya udhibiti wa bidhaa zinazoingizwa au kusafirishwa bila kufuata taratibu za kisheria za forodha.

Bidhaa hizo zilizokamatwa zimehifadhiwa katika yadi ya TRA Bagamoyo kwa ajili ya kuendelea na taratibu za kiforodha na hatua nyingine za kisheria.

Mamlaka ya Mapato Tanzania imeendelea kutoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufuata sheria na taratibu za kodi na forodha ili kuepuka hasara na adhabu zinazoweza kujitokeza.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post