WASANII WAKONGWE WATIKISA USIKU WA TUZO ZA MUZIKI 2021

 

Na John Mapepele

Wasaniii mbalimbali leo Aprili 2, 2022 wakiongozwa na Bendi  iliyowaunganisha wanamuziki kutoka Chama cha Muziki wa Dansi nchini (CHAMUDATA)  wamepamba usiku wa   utoaji wa tuzo hizo.
Wanamuziki hao nguli wamepanda jukwaani mara baada ya tuzo za heshima kutolewa.
Mbali na Bendi hiyo kikundi cha wasanii chipukizi na wanamuziki nguli  kadhaa wameburudisha katika tukio la leo ambapo jumla ya  tuzo 51 zinatolewa.
Akitoa hotuba yake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amelitaka BASATA  kuwaunganisha wasanii na kusaidia wasanii wasiibiwe kazi zao  huku akiitaka COSOTA kuwa kuwasajili na kuwasaidia wasanii kupata mirabaha yao  kwa kazi zao zinazotumika ndani na nje ya nchi.
Tuzo za leo zimevuta hisia kubwa kwa wapenzi wa muziki kutokana na ukweli kuwa  Serikali imezifufua baada ya kutokuwepo kwa zaidi ya miaka sita.
Shughuli hii imehudhuriwa  pia na Naibu Waziri. Mhe Pauline Gekul, Katibu Mkuu.Dkt Hassan Abbasi na wadau mbalimbali wa sanaa

Post a Comment

Previous Post Next Post