Na Mustafa Leu.
COSTECH Tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia,muhimili na nguzo kuu ya taasisi za utafiti wa maswala yote ya Sayansi nchini imejizatiti kuhakikisha wananchi wananufaika na uguduzi na utafiti unaofanywa na wanasayansi nchini na Kuharakisha mabadiliko yaharaka ya maendeleo kwajamii ..
Kwa kipindi kirefu Utafiti na ugunduzi wa maswala mbalimbali ya kisayansi umekuwa ukifanyika maeneo mbalimbali nchini lakini umekuwa ni siri kubwa ambayo imeshindwa kuwafikia walengwa na hivyo kushindwa Kuleta mabadiliko yaliyokuwa yakitarajiwa kwa wakati.
Zipo changamoyo ,mbalimbali ambazo zimesababisha matokeo ya tafiti hizo kutokuwafikia walengwa,ikiwemo lugha ngumu ya kitaalamu iliyotumika kuandika taarifa nayotumika na matokeo yake taarifa hizo kubakia siri ya watafiti
Kaimu mkurugenzi mkuu wa COSTECH, Daktari,Philibelrti Luhuga,anasema kutokana na changamoto hiyo ya matokeo ya utafiti kutokuwafikia walengwa na hivyo kuleta mabadiliko taasisi hiyo imekuja na suluhisho la kudumu
COSTECH,Imeamua kushirikisha na. kutumia vyombo vya habari ili viweze kuandika taarifa za matokeo hayo kwa lugha rahisi inayoeleweka kwa walengwa na hivyo matokeo ya tafiti na gunduzi yataleta mabadiliko ya haraka
Vyombo vya habari vikiwemo,radio,luninga majarida,magazeti,vipeperushi,
Tunawapongeza COSTECH kwa uamuzi wao wa kuvishirikisha vyombo vya habari hayo ni mafanikio makubwa Katika utafiti ugunduzi na. ubunifu yatawezesha kupatikana matokeo ya haraka amboyo taifa linayangojea
Tayari wanahabari mikoa mbalimbali wameshaanza kunolewa na wengine wanaendelea kunolewa ili wawe na uelewa mkubwa wa maswala yatafiti na ugunduzi hayomar waandike kwa lugha nyepesi ambayo inaeleweka.
Watafiti hawapaswi kulaumiwa kwa kushindwa kutoa matokeo ya tafiti huo ni mfumo uliokuewepo tangia kale kwa kuwa umejengwa Kama mtafiti akisha kamilisha utafiti wake anauwasilisha kwenye mamlaka husika na yeye hana nafasi au jukumu la kuelezea popote.