WAZIRI JAFO ATOA MAELEKEZO KUEPUSHA ATHARI ZA KIMAZINGIRA WILAYANI PANGANI

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wananchi Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara ya kukagua changamoto za kimazingira katika Mto Pangani ambao unatishia kula sehemu ya ardhi ya wananchi wa Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (mwenye koti mbele) akikagua kingo za Mto Pangani ambao unatishia kula sehemu ya ardhi ya wananchi wa Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifafanua jambo wakati wa ziara ya kukagua changamoto za kimazingira katika Mto Pangani ambao unatishia kula sehemu ya ardhi ya wananchi wa Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (mwenye koti) akiwa katika kivuko kutokea eneo la Bweni kuelekea Pangani Mjini baada ya kufanya ziara ya kukagua changamoto za kimazingira katika Mto Pangani ambao unatishia kula sehemu ya ardhi ya wananchi wa eneo hilo leo Januari 16, 20022. Pembeni yake mwenye jezi ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Pangani, Mwalimu Hassan Nyange.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

………………………………………………………

Na Robert Hokororo, Pangani

 wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara katika Wilaya ya Pangani mkoani Tanga leo Januari 16, 2022 kukagua athari ya kumomonyoka kwa ardhi katika ukingo wa Mto Pangani eneo la Bweni.

Akiwa katiia ziara hiyo Dkt. Jafo ametoa maelekezo kwa kwa afisa mazingira wa wilaya na mkoa kwa kushirikiana na wataalamu wa ujenzi kufanya tathmini ya namna gani ya nini kifanyike ili Serikali iweze kutafuta fedha kunusuru changamoto hiyo.

“Hili jambo nimelichukua na niwaahidi nitaenda kulifanyia kazi na natoa mwezi mmoja kwa afisa mazingira kwa mkoa na wilaya pamoja na mainjini muende mkafanye tathmini ni kiasi gani cha fedha kitahitajika ili kuparekebisha mahali hapa,” alisema.

Aidha, Waziri Jafo alisema kuwa eneo hilo lina changamoto kubwa kiasi cha kuweza kuhatarisha maisha ya wananchi na hata pengine kutishia kukatisha mawasiliano ya barabara wakati wa kipindi cha bamvua.

Alipongeza na kushuruku taasisi wilayani humo kwa kushirikiana na Serikali kupanda mikoko kando ya Mto Pangani kiasi cha takriban 24,000 zaidi ya lengo la 21,000 walilojiwekea.

Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi waitunze mikoko hiyo ili iweze kuwa na manufaa hususan katika kusaidia jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Wilaya ya Pangani, Bw. Daudi Mlahagwa akiwasilisha taarifa ya mazingira alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya vyanzo vya maji.

Alibainisha kuwa miongoni mwa changamoto hizo ni kukauka kwa baadhi ya vyanzo hivyo, wafugaji kuingiza mifugo katika vyanzo na hivyo kuviharibu, visima vifupi kukauka kutoka na joto kali na chumvi kuingia katika visima na kusababisha kutokufa kwa matumizi ya binadamu.

Post a Comment

Previous Post Next Post