DAWASA YAPELEKA SHANGWE YA MAJI MBAGALA

 Na Humphrey Shao, Michuzi Tv



Baada ya taabu ya muda mrefu ya kukosa maji masafi, wakazi wa Makuka kusini, kata ya Mbagala Jijini Dar es Salaam wameanza kupata maji kwa mara ya kwanza.

Neema hiyo imewafikia baada ya jitihada kubwa za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kutekeleza mradi wa maji kwa kutumia fedha za ndani na kufikisha maji kwa wakazi hao.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa mradi wa maji Makuka Kusini, Msimamizi wa mradi Hassan Mnga'la kutoka DAWASA amesema mradi unawafikia wakazi takribani 3,600 wa eneo hilo.

"Kazi ilihusisha ujenzi wa vituo vya kuchotea maji ili kila mwananchi aweze kupata maji," ameeleza.

"Lengo la ujenzi wa vituo hivi vya kuchotea maji ni kumwezesha mwananchi wa hali ya chini kupata maji kwa urahisi," amesema.

"Tumetambua tabu waliyokua wanaipata wananchi wa Makuka, kwani ni muda mrefu hawakua na maji, lakini kwa sasa ni dhahiri kwamba shida ya ukosefu wa maji imeisha," amesema.

Wema Pogolwa Mwenyekiti wa mtaa wa Makuka Kusini amesema anaishukuru sana Mamlaka kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuleta maji kwenye mtaa huu.

"Wakazi wa mtaa huu wamekua kwenye shida ya ukosefu wa maji kwa muda mrefu maana hapakupa na mradi wa kusambaza maji, hivyo wengi walikua wakitumia maji ya visima yenye chumvi," ameeleza.

Tunaipongeza sana serikali kupitia DAWASA kwa kutekeleza mradi huu wenye manufaa kwa wananchi hawa.

Kwa upande wake Mkazi wa Makuka kusini Furaha Mwenda amesema kuwa maji wanayopata kutoka DAWASA ni mazuri na matamu, na hayana matatizo ya kiafya.

"Apo zamani tulikua tunanunua maji kwa watu binafsi kwa gharama kubwa ya sh mia mbili kwa lita ishirini na wengi hawakua wanachemsha hivyo kuhatarisha afya zao," ameeleza Mwenda.

Mariam Mwingira, mkazi wa Makuka amesema kuwa awali majiasafi hayakwepo, "tulikua tunatumia maji ya watu binafsi ambayo hayakua yakipatikana kwa uhakika," ameeleza.

"Kwa sasa tunashukuru maji ya DAWASA kuja yanatusaidia kupunguza changamoto ya kupatikana kwa maji," amepongeza.
Mmoja wa Watangazani Maarufu nchini kutoka kituo Cha Radio Cha EFM Dina Marios akimtua ndoo mama kichwani kama ishara ya kuonesha kuwa sasa mateso basi ya kusafiri umbali mrefu kufuata Maji.
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Makuka Kusini Mbagala wakifurahia huduma ya maji yaliyofunguliwa na Dawasa

Post a Comment

Previous Post Next Post