WANANCHI MKOANI RUKWA WATAKIWA KUSHEREHEKEA SIKUKUU KWA AMANI NA UTULIVU

 

********************

Sumbawanga, 24 Desemba, 2021

Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wametakiwa kusheherekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2022 kwa amani na utulivu huku wakiendelea kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

Mkuu wa Mkoa huo Mheshimiwa Joseph Mkirikiti ametoa wito huo leo (24.12.2021) wakati akitoa salamu zake za heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2022 kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake mjini Sumbawanga.

“ Napenda kwa niaba ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa niwatakie salamu za heri na baraka wananchi wote katika kusheherekea sikukuu ya Krismasi .Tusheherekee kwa amani ,upendo na umoja . Niwatake pia tuwe watulivu na tuhakikishe watoto hawaendi kwenye maeneo hatarishi kwa afya na usalama wao “alisisitiza Mkirikiti.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kusema Jeshi la Polisi tayari limetoa maelekezo kuonya dhidi ya wote watakaojihusisha na uvunjifu wa amani na kuwa wananchi wawe tayari kutoa taarifa endapo watabaini vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani

Post a Comment

Previous Post Next Post