GEKUL-DROO YA UPANGAJI WA MAKUNDI YA TIMU NA RATIBA TAIFA CUP YATOKA

 

Shafi Dauda (kushoto) na Baraka Kizuguzo ambaye ni Afisa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) wakichezesha droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano ya Taifa CUP 2021

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul akishuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam. Kushoto Kaimu Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa. Bi Neema Msita, kulia Mkurugenzi wa Michezo. Yusu Omary Singo.

Wadau wa michezo wakishuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam.

********************

Na. John Mapepele

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul leo, Disemba 8, 2021 ameshuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika tukio hilo amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kurejesha mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesimama kwa miaka kadhaa.

Aidha, amesema mashindano ya mwaka huu yameboreshwa tofauti na yale ya awali.

Amesema maboresho hayo ni pamoja na kuingiza michezo mitatu; soka kwa wanaume na wanawake, netiboli na riadha kwa wanaume na wanawake ambapo awali ulikuwa mchezo mmoja tu wa soka.

Pia amesema mashindano haya yameshirikisha pande zote mbili za Tanzania ili kuwa na sura ya kitaifa Ametoa rai kwa vyama vya michezo na mashirikisho kuja kwenye mashindano hayo ili kuona vipaji vya wachezaji ambao wanaweza kuwachukua kwenye vilabu vyao.

Akizungumzia dhana ya Taifa CUP amesema lengo la mashindano hayo ni kuwashirikisha wanamichezo kutoka mikoa yote nchini ambapo amesisitiza kuwa mashindano hayo yanasaidia kuleta umoja na mshikamano, kutoa ajira na kuimarisha afya za wachezaji hao.

Akimkaribisha Mhe. Gekul kutoa hotuba fupi kabla ya kuchezesha droo hiyo Mkurugenzi wa Michezo nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandlizi ya Taifa CUP, Yusufu Omary Singo amesema droo hiyo imechezeshwa kwa uwazi ili kuyafanya yawe wazi zaidi

Post a Comment

Previous Post Next Post