No title

  

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti  akiwa na Wazee wa Sumbawanga ambao kati yao walikuwepo siku ya Desemba09,1961 wakati bendera ya Uingereza  ikishushwa na kupandishwa bendera ya Tanga huru eneo la Bomani Sumbawanga. Eneo hilo patajengwa mnara wa kumbukumbu ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
……………………………………………………
Katika kuadhimisha sherehe za uhuru wa Tanzania Bara leo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akiwa na Wazee wa Mji wa Sumbawanga wamezindua jiwe la msingi la mnara wa kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru mahala ambapo bendera ya Tanganyika huru ilipandishwa mara ya kwanza Desemba 09 ,1961.
Tukio hilo limefanyika leo (08.12.2021) eneo la Bomani wilaya ya Sumbawanga  ambapo Mkuu huyo wa Mkoa akiwa na wazee ambao walikuwepo siku ya uhuru mwaka 1961 .
Eneo hilo lililopo jirani na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga  patajengwa mnara huo mapema mwaka huu ili iwe ni kumbukumbu muhimu kwa vizazi vijavyo.
Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru Kimkoa yanafanyika kijiji cha Kaengesa Wilaya ya Sumbawanga ambapo mkoa wa Rukwa unajivunia uwepo wa maendeleo makubwa ya elimu ,miundombinu pamoja na uwepo wa nguvu kazi mahili yenye utayari wa kufanya kazi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti  wa Baraza la Wazee Manispaa ya Sumbawanga  Joseph Ngua aliomba uongozi wa mkoa huo ufanye jitihada za kurejesha historia ya Sumbawanga  kwani mwaka 1960 Mwalimu Julius Nyerere alifika Sumbawanga na kuongea na wazee hao kuhusu harakati za uhuru.
” Tunaomba serikali itunze historia ya eneo hili la Bomani mahala ambapo bendera ya mkoloni wa Uingereza  ilishushwa na kupandishwa bendera ya Tanganyika huru ” alisema Mzee Ngua

Post a Comment

Previous Post Next Post