Waziri Bashungwa Afanya Tathimini Mechi Ya Burundi, Aipa Tanzanite Silaha Za Maangamizi Mechi Ya Ethiopia

 Na John Mapepele, WUSM



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza timu ya Taifa ya wanawake U20 ya Tanzanite kwa kuendelea kufuzu tiketi ya kucheza mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2022 nchini Costa Rica baada ya kushinda goli 1-1 na timu ya Burundi licha ya kucheza wachezaji pungufu( wachezaji nane tu) disemba 18, 2021 nchini Burundi.

Kufuatia ushindi huo leo disemba 21, 2021ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuijenga kimwili na kisaikolojia kuelekea mchezo unaifuata dhidi ya timu ya Ethiopia mapema Januari 2022.

“kwa niaba ya Serikali ninawapongeza sana kwa kuwa mliishangaza Afrika na Dunia, mlicheza pungufu lakini bado tukapata ushindi wa heshima, jambo muhimu kwa sasa ni kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo mechi inayofuata januari na kazi iendelee" amefafanua Mhe. Bashungwa, leo Desemba 21, 2021 alipokutana na timu pamoja na kamati ya ufundi na kufanya tathimini mchezo huo

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanamichezo na timu zote zinazoipeperusha vema bendera ya taifa.

Awali akielezea baadhi ya changamoto walizokabiliana nazo huko Burundi, Mkuu wa msafara wa timu ya Tanzanite Bukuku Mrisho amesema, licha ya sheria za mpira kutaka majibu ya vipimo vya magonjwa mbalimbali kuwasilishwa masaa mawili kabla ya mchezo lakini wao waliletewa majibu ya vipimo vya Uviko 19 wakiwa uwanjani tayari na hata wakati mchezo ukiendelea wataalamu waliendelea kuleta majibu ya vipimo kwa viongozi mbalimbali wa timu.

Katika mchezo wa awali dhidi ya timu ya Burundi uliofanyika jijini Dar es Salaam timu ya Tanzanite iliibamiza Burundi mabao 3-2.





Post a Comment

Previous Post Next Post