TANESCO YAIBUKA KINARA TUZO ZA NBAA

 

Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza katika kutayarisha mahesabu kwa viwango vya kimataifa mwaka 2021 katika kundi la Mashirika ya Umma, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalizaji Umeme TANESCO Mhandisi. Pakaya Mtamakaya akiwa upande wa kulia katika hafla iliyofanyika katika kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mkuu wa Fedha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Renata Ndege (kulia) akishika tuzo ya mshindi wa kwanza katika kutayarisha mahesabu kwa iwango vya kimataifa mwaka 2021 katika kundi la Mashirika ya Umma iliyotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam.

Watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiwa katika hafla ya ugawaji tuzo kwa taasisi mbalimbali zilizofanikiwa kufanya vizuri katika kuandaa taarifa ya fedha kwa viwango vya kimataifa, tuzo hizo zimeandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA)

TANESCO YAIBUKA KINARA TUZO ZA NBA

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefanikiwa kuibuka kinara kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza katika kutayarisha mahesabu kwa viwango vya kimataifa mwaka 2021 katika kundi la Mashirika ya umma inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

CPA. Mkude amesema kuwa taarifa bora za fedha ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi kwa kuwa walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine hutegemea taarifa hizo katika kufanya maamuzi.

CPA. Mkude ni mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji tuzo, amewapongeza washindi wote kwa kupata tuzo baada ya kufanya vizuri kwa kutoa taarifa ya fedha kwa ubora unaotakiwa.

Afisa Mkuu wa Fedha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Renata Ndege, amesema kuwa ni mara ya tano wanashika nafasi ya kwanza kwa kutayarisha mahesabu kwa kutumia kiwango cha kimataifa katika kundi la mashirika ya umma.

Bi. Ndege amesema kuwa kupata tuzo hiyo imetokana na TANESCO kufata utaratibu wa viwango katika kutayarisha mahesabau ya fedha za watanzania kwa salama.

“Tutahakikisha tunaendelea tufata vigezo vinavyotakiwa wakati tunatayarisha mahesabu, huduma zitaendelea kuboreshwa ikiwemo umeme unakuwa wa uhakika “ amesema Bi. Ndege.

Amefafanua kuwa hakuna njia ya mkato ili uweze kupata ushindi pamoja na zawadi, kwani ni lazima ufate taratibu za mahesabu ili uweze kushinda katika mashindano haya.

“Taasisi nyengine zinatakiwa kuwa na uongozi bora pamoja na kufata utaratibu wa mahesabu ili waweze kufanya vizuri zaidi na kuapata tuzo” amesema Bi. Ndege.

Bi. Ndege ameishukuru serikali kwa kufanya uwekezaji wa miundombinu ya umeme ili kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kupatikana wakati wote.

Tuzo za NBAA zinalengo kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kimataifa, ambapo washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu hapa nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha Hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post