WAZIRI BITEKO- SERIKALI KUJA NA MUAROBAINI WA SAKATA LA UCHIMBAJI KWA KAMPUNI YA PUGU KAOLIN MINES LTD

 

******************************
Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko ameingilia kati sakata la zuio la mwekezaji Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Kaolin (Pugu Kaolin Mines Ltd )ambayo hifadhi ya msitu wa Kazimzumbwi wilaya Kisarawe Mkoani Pwani imeizuia kufanya uwekezaji huo miaka sita sasa.
Aidha amesema Serikali itatoa majibu endapo kama kampuni hiyo ifanye shughuli za uchimbaji ama la baada ya Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi kutaka kampuni hiyo isifanye shughuli hizo ndani ya hifadhi hiyo kuepuka uharibifu wa mazingira.
Waziri Biteko amesema hayo, baada ya kutembelea eneo hilo ambalo liko kwenye kata ya Kimani wilaya ya Kisarawe ,eneo lenye utajiri mkubwa wa Caolini na linakisiwa kuwa na tani milioni 800 ni nyingi sana ambazo haziwezi kumalizwa kwa haraka. 
Ameeleza, eneo hilo linaitwa Mwambisi ambapo kampuni inaitwa Pugu Kaolin Mines Ltd ilikuwa ikitaka kuchimba Madini ya Kaolini ambayo ni bora duniani yanayotumika kutengeneza malumalu, kwenye viwanda vya Keda cha Chalinze na Mkuranga .
“Eneo hilo lina utajiri mkubwa, linakisiwa kuwa na tani milioni 800 ambazo ni nyingi ambazo haziwezi kumalizwa kwa haraka”
 ila kuna mazonge mengi yanatakiwa yaishe ,utafiti hapa ulifanyika miaka 1890 enzi za mkoloni na wengine wamekuja kwa tafiti mbalimbali lazima ifike mahali mambo hayo yafike mwisho”.
“Haiwezekani kamati mbalimbali zinakuja wanalipana posho tu, na wameshakuja viongozi wengi lazima jambo hili lifike mwisho kama hii biashara hatuiwezi tusema ,,na kama inawezekana tulimalize ili kazi ianze”anafafanua Biteko.
Hata hivyo ameeleza, Taratibu zifuatwe Kwani zuio huwa ni kwenye hifadhi za Taifa Tanapa za wanyamapori lakini kwenye hifadhi za misitu haijazuia bali taratibu zifuatwe na Tanzania inakadiriwa kuwa na mahitaji ya tani 120,000 kwa mwaka ambapo viwanda vinatumia kati ya tani 70 hadi 80 ambapo  kuna upungufu wa tani 40 kwa ajili ya uzalishaji viwandani kwa ajili ya utengenezaji wa marumaru.
Biteko amesema kuwa baadhi ya maeneo ya uchimbaji yako kwenye hifadhi za misitu lakini kuna taratibu ambazo zinapaswa kufuatwa ili kufanya uchimbaji.
Anasema inashangaza kuona mkuu wa wilaya , viongozi wa Chama ,madiwani hawajui changamoto hizi , hivyo inapaswa pande zote zijue na siyo  Waziri pekee.
“Kikubwa kinachotakiwa ni utaratibu ufuatwe kwani kuliko zuiliwa ni kwenye hifadhi za TANAPA za wanyamapori Lakini sio kwenye hifadhi za misitu haijazuia .”alisisitiza Biteko.
Nae mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon alisema kuwa wanasubiri tamko ili kujua hatma ya eneo hilo kwani mbali ya kuingiza mapato pia litatoa ajira kwa vijana.
Amefafanua ni vizuri suala hilo likafika mwisho ili eneo hilo liweze kutumika kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi na yatolewe maamuzi ambayo yatakuwa na manufaa kwa pande zote.
Kwa upande wake ,Douglas Mwela ofisa Mazingira wilaya ya Kisarawe alisema ,wilaya hiyo ina migodi sita ya machimbo ya Madini hayo ambapo kwenye bajeti ya mwaka 2019/2020 Madini hayo yaliingizia Halmashauri kiasi cha sh.milioni 270 na mwaka 2021 yaliingiza milioni 288 ambapo madini ya Kaolin yanayotumiwa kwenye viwanda vya Keda cha Chalinze na Mkuranga vyote vya marumaru ndiyo vinatumia Madini hayo ambayo ni bora duniani. 
Mwela alisema hadi robo ya pili ya bajeti ya mwaka 2021/2022 tayari wamekusanya kiasi cha sh.milioni 99 na mgodi huo ulikuwa chini ya shirika la madini stamico na uzalishaji ulikoma tangu mwaka 1997.
Mmiliki wa eneo hilo kupitia kampuni ya Pugu Kaolin Mines Ltd Robert Damian alisema kuwa ilikuwa sehemu ya msitu na kubadilishwa nakuwa ardhi ya jumla na kufuata taratibu zote na hawakupewa umiliki na wizara ya ardhi baada ya watu wa msitu TFS kusema uchimbaji huo hauhifadhi mazingira.
Alisema watu wa mazingira walisema kuwa wasiwape vibali kutokana na eneo hilo kuwa la hifadhi ya msitu ambapo wao wanashangaa ambapo sehemu nyingine za uchimbaji ziko kwenye maeneo ya misitu.

Post a Comment

Previous Post Next Post