Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa kuhusu ujenzi wa tenki la kuhufadhia maji linalojengwa Kigamboni wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa mradi huo leo katika wilaya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari kuhusu serikali ilivyojipanga kusimamia miradi ya maji hasa kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi hiki cha upungufu wa maji katika Mto Ruvu wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Kigamboni utakavyoweza kuhudumia kata 7 za Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa akizungumza kuhusu namna waliya ya Kigamboni watakavyoweza kusimamia mradi ili kuweza kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo leo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ya kukagua mradi wa maji wa Kigamboni leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanavyosimamia mradi wa Ujenzi wa Tanki la kuhufadhia maji litakalokuwa na ujazo wa milioni 15 ulipofikia wakati wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ya kukagua mradi wa maji wa Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa wakikagua ujenzi wa tenki la kuhufadhia maji litakalokuwa na ujazo wa milioni 15 za maji kutoka kwenye visima mbalimbali vilivyochimbwa katika Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Mafundi wakiendelea na ujenzi
Muonekano wa tenki la kuhufadhia maji litakalokuwa na ujazo wa milioni 15 lililofikia kwenye ujenzi.