MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU DAWASA YAZINDULIWA RASMI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE.

Lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuleta hamasa na motisha miongoni mwa watumishi na kuimarisha afya ya mwili na akili.

Akizungumza wakati wa akizindua mashindano hayo Mhandisi Luhemeja amesema michezo hiyo itahusisha mikoa 23 ya kihuduma DAWASA pamoja na watumishi kutoka mitambo yote ya uzalishaji maji.

Amesema kuwa mechi ya ufunguzi zitawakutanisha watumishi wa DAWASA kutoka  Mtambo wa Ruvu Juu na Ruvu Chini,  na mechi nyingine itakuwa kati ya Watumishi wa DAWASA Makao makuu dhidi ya DAWASA Temeke mnamo tarehe 6 Novemba 2021.

Ameongeza kuwa katika mashindano hayo zitatolewa zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwa ni pamoja na kombe la dhahabu, medali ya dhahabu pamoja na fedha taslimu Tsh.200,000 kwa wafanyakazi wote wa kituo kitachoibuka mshindi wa  kwanza huku zawadi ya mshindi wa pili itakuwa medali ya Shaba pamoja na fedha taslimu Tsh 100,000 kwa kila mfanyakazi wa kituo kilicholeta ushindi huku mshindi wa tatu atapokea fedha taslimu Tsh. 50,000 kwa kila mfanyakazi wa kituo kilicholeta ushindi.

Washindi binafsi watazawadiwa Tsh.200,000 kwa mfungaji bora, Tsh.100,000 kwa golikipa bora pamoja na Tsh. 100,000 kwa mchezaji bora. 

Tamati ya DAWASA PREMIER LEAGUE itafanyika Januari 8, 2022 katika viwanja vya Chuo cha Sanaa na Utamaduni ADEM wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE leo tarehe 1 Novemba 2021 na yatakayofikia tamati tarehe 8 Januari 2022 ambapo fainali itafanyika kwenye viwanja vya chuo cha ADEM Bagamoyo mkoani Pwani wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bernadetha Mkandya wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu za DAWASA mara baada ya kuzindua mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE leo tarehe 1 Novemba 2021 na kufikia  tamati tarehe 8 Januari 2022 wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimkabidhi kombe Msimamizi wa Mashindano Bakari Makilagi mara baada ya kuzindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE leo tarehe 1 Novemba 2021 wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na watumishi  wa Mamlaka hiyo wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha kwa DAWASA pamoja na kuweka malengo mbalimbali. kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Usimamizi wa DAWASA, Paul Sulley akizungumzia kuhusu tathmini ya robo ya kwanza ya Mwaka wa fedha wa Mamlaka hiyo wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimtambulisha rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bernadetha Mkandya wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bernadetha Mkandya akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hivyo kuhusu namna Mamlaka ilivyojipanga kusimamia wafanyakazi wa ngazi zote ili kuweza kuongeza ufanisi kwenye mamlaka hiyo wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Meneja wa mikoa ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wakifuatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakifuatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post