BAGAMOYO FESTIVAL: WASANII WAKIONGOZWA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA TAMADUNI,SANAA NA MICHEZO WAFANYA ROYAL TOUR KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

 

*********************

Viongozi mbalimbali nchini wakiongozwa na Katibu Mkuu-Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah, wameongoza wadau mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii katika eneo la Bagamoyo na Mkoa wa Pwani. Ziara hiyo pia imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Kennan Kihongosi.

Ziara hiyo iliyolenga pia kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii na uwekezaji nchini, iliitwa jina la Bagamoyo Royal Tour na iliwavutia wasanii wa fani mbalimbali kama vile muziki, filamu, sanaa za ufundi, urembo na waandishi wa habari.

Wakiwa Bagamoyo mjini wadau hao walitembelea eneo la Kaole ambapo wasanii na viongozi hao walipata baraka ya maji ya kisima cha Kaole na kuzuru mti unaoaminika kuongeza uhai.

Nje kidogo ya Bagamoyo kundi hilo likafanya “Royal Tour” kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan iliyoko pembezoni mwa Bahari ya Hindi ambako walifanya utalii wa baharini kwa kutumia boti.

“Sekta za Utamaduni na Sanaa zina mchango mkubwa katika kuvutia watalii; leo nasisi tumetoa mchango wetu katika hilo,” alisema Dkt. Abbasi anbaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania Kimataifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post