TBS YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA VIUNGO VYA VYAKULA JIJINI DAR ES SALAAM

 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ludigija (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Upimaji na ugezi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Johanes Maganga (Kushoto) na upande wa kulia ni Meneja wa Mafunzo na Utafiti katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mwl.Hamisi Mwanasala katika mafunzo kwa wazalishaji na wauzaji wa viungo vya vyakula yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mafunzo na Utafiti katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mwl.Hamisi Mwanasala akizungumza katika mafunzo kwa wazalishaji na wauzaji wa viungo vya vyakula yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Upimaji na ugezi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Johanes Maganga akizungumza katika mafunzo kwa wazalishaji na wauzaji wa viungo vya vyakula yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ludigija akizungumza katika mafunzo kwa wazalishaji na wauzaji wa viungo vya vyakula yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

Washiriki wa mafunzo ambao ni wazalishaji wa viungo vya vyakula wakifuatilia mafunzo  hayo yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Mafunzo hayo yamefanyika leo Jijini Dar es salaam.

Meneja wa Mafunzo na Utafiti katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mwl.Hamisi Mwanasala akiwasilisha mada katika mafunzo kwa wazalishaji na wauzaji wa viungo vya vyakula yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO

***************************

NA EMMANUEL MBATILO

Azma ya Serikali ni kuhakikisha nchi inajitosheleza katika uzalishaji wa bidhaa kwa soko la ndani na hata nje ya nchi, hivyo viungo vinavyozalishwa hapa nchini vinahitajika kwa masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo leo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ludigija akifungua mafunzo kwa wazalishaji wa viungo vya vyakula kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla.

Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika Mkoa huo Mhe. Ludigija amesema kuwa uzalishaji,uuzaji na usambazaji wa viungo vya vyakula ni sehemu ya shughuli kuu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara katika mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Mhe.Ludigija amewataka wazalishaji hao kuzalisha viungo vinavyozingatia viwango, ubora na usalama ili  kulinda afya ya mlaji na zaidi kuongeza soko la viungo  katika nchi za jirani.

“Mafunzo hayo ni njia muafaka wa kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea taifa letu maendeleo  ya  haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya viwanda,kilimo,biashara,uvuvi na maeneo mengine mengi”. Amesema Mhe.Ludigija.

Nae Mkurugenzi wa Upimaji na ugezi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Johanes Maganga akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TBS, amesema katika mafunzo hayo yanajumuisha washiriki  wapatao  100 kutoka katika maeneo  mbalimbali ya mkoa, walengwa wakiwa ni wajasiriamali ambao wanajihusisha na usindikaji, uchakataji na ufungashaji pamoja na uuzaji wa viungo vya vyakula.

Amesema katika mafunzo hayo yatarahisisha kukuza wigo wa masoko yetu na kuongeza pato la Taifa.

Pamoja na hayo amesema kuwa TBS itaendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo kwa wazalishaji, wauzaji na wasambazaji wengine wa viungo vya vyakula katika mikoa.

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo amesema mafunzo hayo yatawapa uelewa mkubwa katika uzalishaji wa viungo kwani wengi wao wamekuwa hawana uelewa ni namna gani wanaweza kuzalisha viungo katika ubora unaotakiwa na kuweza kukuza  soko lake na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post