TBS YATOA LESENI YA KUTUMIA ALAMA YA UBORA KWA WAJASIRIAMALI

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt.Athuman Yusuf Ngenya akimpatia leseni ya kutumia alama ya ubora ya uunganishaji wa mabasi Bw.Jonas Nyagawa kutoka kampuni ya BM Motors iliyopo mkoani Pwani. TBS inatoa leseni hiyo kwa mara ya kwanza Tanzania kwa Kampuni ya kitanzania inayojishughulisha na uunganishaji wa mabasi nchini.

Meneja wa Uthibitishaji ubora Bw.Gervas Kaisi akizungumza na wazalishaji waliohudhuria hafla ya utoaji leseni mapema leo, TBS Ubungo jijini Dar es salaam.
Kaisi alitoa wito kwa wazalishaji hao kuhakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa bora wakati wote ili kuendelea kumlinda mlaji na kuunga mkono jitihada za serikali za kuendeleza Viwanda.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt.Athuman Yusuf Ngenya akimpatia leseni ya kutumia alama ya ubora mjasiriamali kutoka kampuni ya Ulanzi Halisi ya mkoani Iringa inayotengeneza pombe ya ulanzi .
Mjasiriamali huyo ameishukuru TBS kwa kupata alama ya ubora na anategemea kupata soko zaidi ikiwemo nje ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt.Athuman Yusuf Ngenya akizungumza na wazalishaji waliohudhuria hafla ya utoaji leseni mapema leo, Makao Makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post