TASUBA YASAINI MAKUBALIANO NA CHUO CHA TAALUMA YA UREKEBISHAJI TANZANIA (TCTA)

Kaimu Mkuu wa Chuo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  (TaSUBa),Gabriel Kiiza akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo. (Kushoto) ni Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) kwa Kiiza  ni Mkuu wa Chuo cha TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani, akifuatiwa na Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.

Kaimu Mkuu wa Chuo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  (TaSUBa),Gabriel Kiiza na Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani wakikabidhiana makubaliano hayo katika hafla ya utiaji saini. (Kushoto) ni Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) ni Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.

Meza kuu,  Maofisa wa Tasuba na wakufunzi tcta
Baadhi ya maafisa wa Magereza  na TaSUBa wakifuatilia tukio la makubaliano katika hafla ya utiaji saini kati ya TaSUBa na TCTA ya kuendesha mafunzo ya sanaa.



Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani akizungumza katika hafla hiyo. (Kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Chuo TaSUBa,Gabriel Kiiza akifuatiwa na Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) ni Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.

 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  (TaSUBa), Gabriel Kiiza na Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani wakionyesha makubaliano hayo katika hafla ya utiaji saini kwa maafisa wa Magereza na TaSUBa (hawapo pichani). Wengine katika picha  (Kushoto) ni Mwanasheria wa TaSUBa, Daniel Awaki na (Kulia) ni Mkuu wa Mafunzo wa TCTA, SP. Mussa Goliama Mpandiko.

                    ...........................................
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeingia makubaliano ya  kuendesha mafunzo ya sanaa na Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA).

Makubaliano hayo yamesainiwa leo katika Chuo cha TCTA Ukonga na wakuu wa taasisi hizo wakilenga kutoa mafunzo ya Sanaa ya Muziki, Uigizaji na Ngoma.

Kaimu Mkuu wa  chuo TaSUBa Gabriel Kiiza alisema makubaliano hayo yatahusisha utoaji wa mafunzo  kwa kipindi cha muda mfupi kisichopungua mwezi mmoja na kisichozidi miezi mitatu kwa kila udahili.

 Alisema mafunzo hayo yatatolewa na kuendeshwa katika madarasa ya TCTA ambapo maktaba pamoja na vifaa vya kujifunzia vitakuwa vya TCTA .

" Endapo TCTA itakuwa na uhaba wa vifaa vya mafunzo, vitaazimwa kutoka TaSUBa tunavyo vya kutosheleza"alisema.

 Kiiza alisema, TaSUBa ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa  kutoa mafunzo ya sanaa, kufanya utafiti na kutoa ushauri katika maeneo ya sanaa na utamaduni hivyo kupitia makubaliano hayo watashirikiana na  TCTA katika kuendesha  mafunzo katika maeneo ya sanaa za muziki, uigizaji na Ngoma. 

Alisema, tasnia ya Sanaa na Utamaduni inahitaji ubunifu ili kuiboresha na kuleta vitu vipya kila wakati, ambapo mbali na kuwa ni burudani   ni sehemu ya ajira rasmi ambayo inahusisha kundi kubwa la vijana ambao ni nguvu kazi katika uchumi endelevu.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha TCTA  Kamishna Msaidizi wa Magereza  Gideon Matani, alisema makubaliano hayo yatakuwa na tija kwa wanafunzi wake kwani watakuwa na fursa ya kutembelea TaSUBa.

"Kabla ya kuhitimu mafunzo angalau mara moja kwa kila udahili watatembelea TaSUBa  ili  kujifunza mazingira ya taasisi hiyo"alisema.

 
Kamishna Matani alisema, ushirikiano huo  ni fursa nzuri ya kupeana uzoefu katika  Sanaa na Utamaduni kwa kuwa TaSUBa wamebobea na wana uzoefu katika utoaji wa mafunzo hayo.

Alisema  chuo cha TCTA awali  kilijihusisha na utoaji wa  mafunzo kwa Askari  sasa kupitia makubaliano hayo watatoa mafunzo kwa askari na raia.


Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ambapo Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Taasisi halali ya Serikali chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post