NAIBU WAZIRI AIPONGEZA TANROADS KUWATUMIA WAKANDARASI WAZAWA

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe.Mwita Waitara (mwenye suti nyeusi), akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Daraja jipya la Selander (TANZANITE), Juni 6,2021.

Mhandisi wa Daraja la Selander (TANZANITE), Lulu Dunia (kulia), akimweleza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara (mwenye suti nyeusi), maendeleo ya Ujenzi wa mradi huo Juni 6, 2021.

Mwonekano wa Daraja jipya la Selander (TANZANITE), Juni 6,2021

……………………………………

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara amepongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), kwa kuwatumia wakandarasi wazawa katika mradi wa ujenzi wa Daraja jipya la Selander (TANZANITE), lililopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa daraja hilo Juni 6,2021, Naibu Waziri Waitara amesema baada ya wataalam kutoka nje kumaliza kazi yao, wakandarasi wazawa wataweza kusimamia miradi mingine mikubwa hapo baadaye.

“Hawa wakandarasi kwa sasa wanapata ujuzi kutoka kwa wageni, tunaamini wageni wakimaliza mikataba yao wazawa watafanya kazi,” amesema Naibu Waziri Waitara.

Amesema mradi wa daraja jipya la Selander umeajiri wafanyakazi wazawa zaidi ya 800, ambao pia wameboresha maisha yao na Serikali inapata kodi zinazolipwa kwa wakandarasi na wafanyakazi wazawa.

“Nimemuuliza Mhandisi hapa ikitokea mkapewa kazi kama hii mnaweza, amenijibu wanaweza, labda tatizo ni mitambo tu,” amesema.

“Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale amesema lengo la kujenga daraja hilo ni kupunguza ama kuondoa kabisa msongamano wa magari ambao unapoteza fedha nyingi zaidi ya dola milioni 4 kwa siku.

“Hebu fikiria unapoteza fedha zaidi ya dola milioni 4 kwa siku kwa sababu ya msongamano wa magari hapa Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Arusha, wewe kama Mtanzania unajisikiaje? Amehoji Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mfugale.

Mhandisi Mfugale amesema ujenzi wa Daraja jipya la Selander umefikia zaidi ya asilimia 70 na wanatarajia litakamilika kwa wakati.

Mhandisi wa daraja hilo, Lulu Dunia amewahamasisha wasichana kusoma masomo ya sayansi, badala ya kuyakimbia

Post a Comment

Previous Post Next Post