MKURUGENZI MKUU TBS DKT NGENYA ATOA WITO KWA WATANZANIA WASINUNUE BIDHAA BILA KUHAKIKISHA INA ALAMA YA UBORA

 

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Dkt Yusuph Ngenya akizungumza na waandishi wa habari

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Dkt Yusuph Ngenya ametoa wito kwa  watanzania wasinunue bidhaa yoyote bila kuhakikisha
kwamba ina alama ya ubora kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Ngenya aliyasema hayo eneo la Mwahako Jijini Tanga
kunakoendelea maonyesho ya nane ya Biashara ambapo alisema hatua hiyo itasaidia
kuwaondolea hasara ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kutokana na bidhaa
wanazonunua kutokuwa na ubora unaotakiwa.

Alisema kwani bidhaa zimekuwa na athari nyingi katika
matumizi ya binadamu hiyo ni muhimu watanzania kutambua kwamba wanaponunua
bidhaa wanapaswa kuzikagua na kuona kama zina ubora unaotakiwa ili kuweza
kuepukana na majanga ambayo yanaweza kuwakuta kutokana na bidhaa  feki.

“Lakini hata katika operesheni zetu ambazo tumekuwa
tukizifanya tunagundua  bidhaa gani
ambazo zinaingizwa kwenye masoko na hazina ubora ikiwemo bidhaa za ujenzi
,vifaa vya umeme vingi vinakuja feki hivyo tujitahidi kuvitambua na kuviondoa
kwenye soko kwani mfano vifaa vya umeme madhara yake vinaweza kushika moto na
kuweza kuharibu mali”Alisema Mkurugenzi huyo wa TBS

Akizungumzia lengo la uwepo wao kwenye maonyesho hayo ya nane
ya biashara alisema wapo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli za
TBS na namna ya kupata huduma zao

“TBS pamoja na mambo megine kwenye maonyesho kama haya
tunawakaribisha wananchi kuweza kuwaelimisha kwa mfano wale wanaotaka kupata
huduma za TBS ikiwemo  bidhaa zao ziweze
kupata alama ya ubora lakini pia tunashughulikia uuzaji wa bidhaa za chakula na
vipodozi kuweza kupata usajili wa shughuli zao”Alisema Mkurugenzi huyo mkuu wa
TBS.

Hata hivyo aliwataka wajasiriamali watengenezaji  wa bidhaa ndogo ndogo ni rahisi kwanza kwenda
sido kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kupata cheti  kitachowawezesha kupata barua kutoka sido na
baadae waende   TBS kuweza kutambulika na
wao watafanya kazi iliyobakia mpaka kuhakikisha bidhaa yao inapata ubora.

Post a Comment

Previous Post Next Post