WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATAJA MIKAKATI YAKE YA KUTANGAZA HIFADHI ZAKE IKIWEMO YA HIFADHI YA KITULO

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akijibu swali la Mbunge wa Makete, Mhe. Richard Francis Sanga leo jijini Dodoma ambapo amesema serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kutangaza vivutio vyote vya utalii nchini pamoja na kurekebisha miundombinu ya maeneo ya uhifadhi ili kurahisisha ufikaji wa Watalii katika maeneo hayo.

********************

Wizara ya Malisili na Utalii imesema mikakati yake iliyo nayo kwa sasa ni kuzitangaza Hifadhi zote za Taifa ndani na nje ya nchi ikiwemo Hifadhi ya Kitulo.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Jijini Dodoma na  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Mhe. Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete,  Mhe. Festo  Sanga   lililokuwa likihoji upi mkakati wa serikali  wa kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ili ifahamike  kwa watalii  ndani na nje ya nchi.

Akijibu swali hilo, Mhe.Masanja amesema Hifadhi ya  Kitulo ni moja kati  ya Hifadhi yenye sifa ya kipekee kwa kuwa na jamii mbalimbali za  maua (Serengeti of Flowers) na kwa kutambua hilo  Serikali imekuwa ikiendelea kuitangaza.

Akijibu swali hilo Mhe. Masanja amesema miongoni mwa mikakati ya kuitangaza  Hifadhi hiyo njia mbalimbali zimekuwa zikitumika  kama ilivyo katika Hifadhi nyingine ikiwemo  kupitia tovuti na mitandao ya kijamii pamoja na kuandaa video na filamu mbalimbali.

Aidha, Amesema ili kuvutia Watalii wengi zaidi Serikali imekuwa ikiimarisha miundombinu ya barabara  ndani ya Hifadhi hiyo kwa  lengo la kurahisisha ufikikaji  wa maeneo ya vivutio vya Utalii.

‘’ Tumeanzisha Chaneli maalumu ya utalii ya “Tanzania Safari Chanel”  pamoja na  kujenga sehemu ya malazi ya bei nafuu ili kuwavutia Watalii wengi kutembelea Vivutio vya Utalii nchini, amesisitiza Naibu Waziri Masanja.

Akijibu maswali ya nyongeza kuhusiana na Uwekezaji katika maeneo ya Hifadhi,  Mhe. Masanja  amesema  Wizara ya Maliasili na Utalii haina  gharama yeyote inayohusiana na uwekezaji, Hivyo amewatoa wito kwa  Wawekezaji  kuja kuwekeza katika maeneo ya  Hifadhi zilizopo 

Katika hatua nyingine, Mhe Masanja amesema serikali imejipanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kuhakikisha inaimarisha Miundombinu katika  maeneo yote ya Hifadhi kwa kutenga  fedha ya kutosha ili kuwavutia Watalii kutembelea maeneo ya Hifadhi. 

Ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka wa fedha  2021/2022 Serikali imezingatia masuala ya utangazaji wa vivutio vya  utalii pamoja na  kuboresha miundombinu ikiwemo barabara,viwanja vya ndege na maeneo ya malazi kwa wageni ili kuvutia watalii kutembelea maeneo hayo kwa urahisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post