TPA WASISITIZWA KUACHA MAJUNGU, MAKUNDI

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akizungumza na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), (hawapo pichani), katika Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, mkoani Morogoro. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Erick Hamisi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Erick Hamisi, akisoma Taarifa ya Utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), katika Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, mkoani Morogoro.

Wajumbe wa Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho (hayupo pichani), katika Kikao cha Baraza cha Mamlaka hiyo, mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Jonathan Msoma, akitoa maoni yake kuhusu kuboresha Mamlaka hiyo, katika Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, mkoani Morogoro.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye tai), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Erick Hamisi (Wapili kushoto) pamoja na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi cha Mamlaka hiyo, mara baada ya kufungua Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi hao, mkoani Morogoro.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), mara baada ya Waziri huyo kufungua kikao hicho, mkoani Morogoro.

PICHA NA WUU

…………………………………………………………………………………………………….

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho, amewataka Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuepuka majungu, fitina na makundi katika maeneo ya kazi na badala yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta ufanisi na tija kwa Mamlaka hiyo naTaifa kwa ujumla.

Akizungumza katika Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, kilichofanyika mkoani Morogoro, Waziri huyo amewasisitiza Wafanyakazi hao kushirikiana katika kupinga vitendo vya wizi na rushwa kwa kufanya kazi kwa weledi na bidii pamoja na kulinda kwa nguvu zote mahusiano mema baina yao.

“Ni imani yangu kwamba katika kutekeleza majukumu yenu mliyopewa na Serikali, mtaendeleza utaratibu wa kushirikiana kati ya Menejimenti na chama chenu cha Wafanyakazi (DOWUTA), kulinda maslahi ya Taifa ndani ya Bandari, kwa kupinga vitendo vya rushwa na wizi”, amesema Chamuriho.

Ameongeza kuwa, kila mmoja anatakiwa kuheshimu nafasi ya kila mtu katika eneo la kazi kwani majukumu yao yanategemeana katika kufikia malengo ya Mamlaka hiyo.

Amewasisitiza wajumbe wa Baraza hilo kutumia kikao hicho, kupitia kwa makini mpango na bajeti yao, kushauri na hatimae kuja kusimamia utekelezaji wake.

Ameitaka Menejimenti  na wawakilishi wa Chama cha wafanyakazi cha Mamlaka hiyo,  kuwajibika kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote wa Mamlaka wanatambua na kutimiza wajibu wao ipasavyo pamoja na kusimamia maadili ya utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi na tija.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Erick Hamisi, amesema tashirikiana na wafanyakazi wa TPA ili kufikia malengo ya Taasisi waliyojiwekea.

Kikao hicho cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPA kina dhima kuu ya kujadili masuala ya bajeti, utendaji, uendeshaji wa bandari na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa na Mamlaka hiyo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post