REA NA TANESCO WAKUTANA DODOMA KUTATHMINI HALI YA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI

 

 Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Mhandisi Amos Maganga,akizungumza na waandisi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kufungua  washa ya siku mbili ya Wahandisi na Mameneja wa Mikoa wenye lengo la kutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dk. Tito Mwinuka,akizungumza mara baada ya kufungua Washa ya siku mbili ya wahandisi na Mameneja wa Mikoa wenye lengo la kutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati vijijini inayofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Washa ya siku mbili ya Wahandisi na Mameneja wa Mikoa inayofanyika jijini Dodoma wenye lengo la kutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini.

………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini REA na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kwa pamoja wamekutana kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya usambazaji wa umeme vijijini kwa awamu ya kwanza, pili na tatu mzunguko wa kwanza kwa lengo la kubaini changamoto kabla ya kuanza kutekeleza awamu inayofuata.

Akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa washa ya siku mbili ya wahandisi na Mameneja wa Mikoa, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA,Mhandisi Amos Maganga amesema wameamua kukutana na wadau wote ikiwa ni watumishi wa REA, wakandarasi, Mameneja wa TANESCO Mikoa na kanda kwa lengo la kutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini.

“Serikali imeweka malengo na mipango yake kuhakikisha wananchi kila Kijiji wanapata nishati bora ya umeme, sasa leo tumekutana hapa lengo ni kuangalia changamoto zote tulizozipata kwenye utekelezaji awamu zilizopita ili tuone namna ya kuzitatua na kuhakikisha vijiji vyote vinapata nishati ya umeme” amesema Mhandisi Maganga.

Amesema katika utekelezaji katika awamu ya kwanza, pili na tatu mzunguzo wa kwanza zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa sana ambapo wamefanikiwa kufikisha umeme mpaka sasa katika vijiji 10,300 sawa na asilimia 87, kati ya vijiji 12,268 vilivyopo hapa nchini na lengo ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata nishati ya umeme.

Ameongeza kuwa “tumekutana leo hapa ni kuangalia tumetoka wapi, tupo wapi na tunakwenda wapi,tumetekeleza awamu hizo tatu changamoto ni nini, ili tunapoanza utekelezaji mradi mkubwa awamu ya tatu mzunguko wa pili changamoto hizo tuziondoe” amesema.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Dkt Tito Mwinuka, amesema warsha hiyo ni ya siku mbili ambayo imewakutanisha REA, TANESCO na wakandarasi ni kushirikishana changamoto walizokutana nazo na kuona vijiji 1,974 vilivyobaki vitafikishiwa vipi umeme.

Amesema hivi sasa wanatarajiwa kuanza utekelezaji wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili ambapo wamedhamiria kuondoa dosari zote zilizojitokeza katika utekelezaji wa REA awamu zilizopita ili kuhakikisha wanafikia lengo la kila Kijiji kupata nishati ya umeme.

Post a Comment

Previous Post Next Post