KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YAPANUA WIGO UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA WAKE NCHINI , VITUO VYAKE VYOTE KUFANYA KAZI SAA 24

 Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania Limeted inayoongoza kwa uuzaji wa mafuta imekuja na mkakati mpya wa kuboresha huduma zake ikiwa pamoja na kusogeza huduma zake karibu na wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.

Mbali ya kupanua wigo wa utoaji huduma zake kwa kuanzisha vituo vipya vya mauzo ya mafuta rejareja katika mikoa ya Kagera(Bukoba), Morogoro (Kihonda) , Dar es Salaam (Kigamboni, Kijichi) Tanga (Segerea).

Aidha kampuni hiyo imebadilisha muonekano wa vituo vyake vya rejareja vya Oysterbay, Upanga .Bagamoyo na Ocean Road jijini Dar es Salaam na kwamba hatua hizo zinalingana na ahadi ya kampuni yenye dhamira yake ya Kuimarisha Jamii ili kukuza ukuaji wa ustawi.

Akizungmza leo Aprili 29,2021 katika Kituo cha Mafuta Oyesterbay jijini Dar es Salaam Meneja Mauzo Rejareja wa kampuni hiyo Vennesy Chilambo amesema hatua ambazo wamechukua wanaamini kabisa hitaji la la kusaidia jamii kwa kufanya upatikanaji wa mafuta na vilainishi vya bei rahisi kwa ubora unaofaa na kiwango sahihi hapa nchini Tanzania.

"Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limeted inataka kufikia kusudi lake la kibiashara kupitia ukuaji wa upanuzi wake ili kuhakikisha kuwa jamii zinanufaika.Aidha kuanzia sasa vituo vyote vya kampuni hiyo nchi nzima vitatoa huduma kwa saa 24.

"Kama inavyofahamika ubora wa bidhaa zetu, tunataka isiishie mijini pekee tunazidi kusogea katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuwafikia watumiaji wa vyombo vya moto," amesema Vennesy.

MENEJA Mauzo ya rejareja wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Venensy Chilambo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 28,2021 katika Kituo cha Mafuta cha kampuni hiyo kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam kuhusu hatua mbalimbali ambazo wamechukua kupanua mtandao wake wa utendaji ikiwa pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya mafuta katika maeneo mbalimbali nchini.Pia amezungumzia jinsi ambavyo kampuni hiyo imeendelea kuboresha utoaji wa huduma zake kwa wateja pamoja na muonekano mpya wa vituo vya mafuta ya Puma.Pichani kulia ni Territory Manager Andrea Laizer na kushoto ni Network Specialist  Alfred Moshi kutoka kampuni hiyo

Post a Comment

Previous Post Next Post