Mkaguzi wa TBS, BW. Colman Venance akimsajili mfanyabiashara wa duka la chakula katika eneo la Manzese jijini Dar es salaam , ikiwa ni mwendelezo wa zoezi la usajili wa majengo ya chakula na vipodozi. Mfanyabiashara Bw.Vicent S. Malandu alipatiwa elimu kuhusu usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi, na aliipongeza TBS kwa huduma nzuri wanayoitoa kwa wadau na kuwataka kufanya hivyo nchi nzima ili kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa mbalimbali.
Tbs limeendelea kuwahamasisha wafanyabiashara, wenyeviwanda na wazalishaji wa bidhaa kusajili bidhaa na majengo yao ili kuweza kuzalisha bidhaa zilizokidhi viwango