………………………………………………………………………………..
. NA FARIDA SAID MOROGORO
Maafisa na Askari wa Uhifadhi wa TAWA wameshiriki katika maandamano ya kusherehekea siku ya wanawake Duniani
Watumishi hao waliongozwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Bi.Gloria Bideberi
Akizungumza katika siku hiyo ya wanawake Mkuu wa wilaya ya
Morogoro Bw.Bakari Msulwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa
fursa na kuwaamini zaidi wanawake na watoto wa kike katika nafasi za
uongozi, siasa, masomo na katika taasisi za umma kwa kuwa siku zote
wameonesha upendo, uchapakazi, uzalendo, umakini na utekelezaji
uliotukuka.
Aidha amesema Serikali imetekeleza kwa kivitendo na itaendelea
kufanya hivyo katika ujenzi wa miradi ya mbalimbali kwani siku ya
wanawake wameendelea kuvunja rekodi ya kushiriki katika kazi mbalimbali
za kujenga Taifa.
Aidha,Kwa upande wa TAWA Kamishna
Msaidizi Mwandamizi Bi.Gloria Bideberi alizungumza na wandishi wa habari
amesema TAWA inaadhimisha siku ya wanawake kwa kushirikiana na taasisi
nyingine huku akitoa wito kwa watumishi wote wanawake kujali na kupenda
kazi zao wawapo kazini.
hatimaye baada ya shughuli hiyo Bi.Groria aliwaongoza watumishi
kwenda kupata vinywaji na kukata Keki ikiwa ni sehemu ya sherehe ya
kujipongeza.