MWAKALINGA AWATAKA WATUMISHI UJENZI KUJITATHIMINI

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akiwasili katika Ukumbi wa mikutano katika Chuo Kikuu cha Dodoma, kwa ajili ya kikao kazi na watumishi wa Sekta yake, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisisitiza jambo kwa watumishi wa Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani) katika kikao kazi, jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Sekta ya Ujenzi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, wakati wa kikao kazi, jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Sekta ya Ujenzi wakijadiliana jambo, kabla ya kikazo kazi cha Sekta hiyo, jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………….

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, amewataka watumishi wa Sekta ya Ujenzi kujiendeleza kitaaluma ili kubobea katika fani zao na hivyo kuleta tija mahali pa kazi.

Akizungumza jijini Dodoma katika kikao kazi cha watumishi wote wa Sekta ya Ujenzi cha kutathimini utendaji kazi, Katibu Mkuu huyo amemtaka kila kiongozi na atumishi kuweka mpango wa kujiendeleza kielimu unaoendana na taaluma zao na mpango mkakati wa Serikali.

“Hakikisheni kila mtumishi anajua majukumu yake, anayatekeleza na anapimwa ili kuwezeshwa katika eneo ambalo ana upungufu na hivyo kuwafanya watumishi wa sekta ya ujenzi kubobea katika maeneo yao”, amesisitiza Arch. Mwakalinga.

Amezungumzia umuhimu wa menejimenti na watumishi kufanya kazi kwa upendo, ushirikiano na kuaminiana ili kufikia malengo kwa wakati.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Ziana Mlawa, amemshukuru Katibu Mkuu huyo kwa utaratibu wake wa kukutana na wafanyakazi mara kwa mara, kuwakumbusha majukumu yao, kuwapa mwelekeo na kutatua changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao.

Zaidi ya watumishi 220 wa Sekta ya Ujenzi wameshiriki kikao kazi hicho na kuahidi kufanya kazi kwa weledi, bidii, na ushirikiano miongoni mwao na kwa wadau wa Sekta ya Ujenzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post