CHAMURIHO AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI (MSCL)

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, jijini Mwanza.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akikabidhi mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza. Wanaopokea kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL, Eric Hamisi na kulia ni Mohamed Rume, mwakilishi wa Katibu Mkuu DOWUTA tawi la Mwanza.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), wakishuhudia makabidhiano ya Mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi yaliyofanywa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL, Eric Hamissi na Mohamed Rume, mwakilishi wa Katibu Mkuu DOWUTA tawi la Mwanza (hawapo pichani), katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho (aliyeketi katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL). Kulia kwa Waziri ni  Mwenyekiti wa Bodi ya MSCL Profesa Zacharia Mganilwa, akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa MSCL, Eric Hamisi. Kushoto kwa Waziri ni  Goodluck Luginge, Afisa Kazi Mkoa wa Mwanza na Mohamed Rume, mwakilishi wa Katibu Mkuu DOWUTA tawi la Mwanza.

Post a Comment

Previous Post Next Post